MABONDIA Twaha Kiduku na Alex Kabangu leo wamekutana kwa mara kwanza na kila mmoja kumchimba mkwara mwenzake kuelekea katika pambano la ubingwa wa UBO Afrika linalotarajia kupigwa keshokutwa Jumamosi mkoani hapa.
Kiduku na Kabangu watapanda ulingoni katika pambano hilo ambalo litachezwa kwa raundi nane katika uzito wa kati ambalo litapigwa kwenye Ukumbi wa Tanzania chini ya Kampuni ya Peak Time Media inayoongozwa na Meja Seleman Semunyu.
Pambano hilo limedhaminiwa na Azam Tv, Global Tv, Championi, Bongo boxing safari, Creative Bee, Smartgin, Magadu Hotel, Roby one Phamarcy na SMH and Logistic Coach huku kiingilio chake kikiwa ni sh 10,000, Sh 20,000 na Sh 30,000 kwa VIP.
Mratibu wa pambano hilo, Bakari Khatibu alisema kuwa maandalizi ya pambano yamekamilika kwa asilimia 100 huku akiwataka wadau wangumi nchini kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo.
“Maandalizi kwa upande wetu ni mazuri tunashukuru Mungu tayari Kabangu ameshaingia na yupo hapa Morogoro, tunachosubiria ni siku kufika kwa ajili ya mambo mengine.
“Lakini nitume nafasi hii kuwashukuru wadhamini wote katika pambano hili ambalo linaenda kuacha historia kubwa ndani ya Morogoro, jambo la kuwakumbusha ni kwamba tiketi zimebakia chache hivyo watu waendelee kujitokeza kununua katika vituo,” alisema Khatibu.
Kwa upande wa mabondia kila mmoja alimtambia mwenzake kua atahakikisha anafanikiwa mkuchapa kutokana na maandalizi walioweza kufanya kuelekea kweye pambano