Na: Costantine James, Geita.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameitaka Migodi kutotiririsha maji taka yenye kemikali katika vyanzo vya maji ili kuwaepusha wananchi kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Ugonjwa wa Saratani.
Alisema hayo wakati alipotembelea mgodi wa dhahabu wa GGM wakati alipokuwa ameambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya ukimwi na kifua kikuu ambapo wanatembelea sehemu mbalimbali ambazo zinakusanya watu wengi kama migodini kwa lengo la kuangalia jinsi wanavyo jikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi na kifua kikuu.
Dkt. Mollel alisema mikoa ya kanda ya ziwa imekuwa ni wahanga wakubwa wa ugonjwa wsa saratani hivyo wanafanya ukaguzi kugundua chanzo ni nini maeneo hayo ya kanda ya siwa kwanini yanawagojwa wengi wa saratani.
“Mikoa ya Kanda ya Ziwa inaonekana kuongoza kwa ugonjwa wa Saratani, tumeamua kufanya utafiti kujua nini kinasababisha tatizo hilo kukua kwa kasi kubwa maana ukija Hospitali ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean Road wagonjwa wengi ni wa Kanda ya Ziwa” alisema Dkt. Mollel.
Kwa upande wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu ilitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Makampuni ya Migodi mbali mbali kuwa na mpango endelevu wa kutoa elimu ya kujingina na magonjwa ya UKIMWI na Kifua Kikuu kwa wafanyakazi.
Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Hassan Toufiq mara baada ya Kamati kutembelea Mgodi wa GGM kuona utekelezaji wa afua mbalimbali za kupambana na UKIMWI na Kifua Kikuu.
Hata hivyo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu imeupongeza Mgodi wa GGM kwa kutoa elimu ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu kwa wafanya kazi wa mgodi huo hali ambayo inasaidia kupunguza maambukizi ya ugojwa huo kazini.
“Hapa tumeona mnafanya vizuri katika kutoa elimu ya kujilinda dhidi ya magonjwa ya UKIMWI na Kifua Kikuu, hongereni sana na sehemu nyingine pia wafanye hivi ikiwa ni pamoja na kuwatunza watu wanaoishi na UKIMWI na Kifua Kikuu” alisema Mhe.Fatma Hassan Toufiq.
Mbunge wa Geita mjini Mhe. Constantine Kanyasu amewatoa hofu wakazi wa Geita juu ya matumizi ya maji ya mvua kutokana na madai ya kuwa maji ya mvua yana vumbi la Zebaki nakusema kuwa maji hayo hayana vumbi yoyote ya zebaki kwani zebaki haiwezi kupaa.
Mhe. Kanyasu amesema serikali kupitia bunge ilipitisha sheria ya kuondoa taratibu matumizi ya zebaki kutokana na athali yake kwenye kansa hasa ukanda wa mikoa ya kanda ya ziwa ambapo imeonekana kansa ni tatizo kubwa.
“Bunge lilipitisha sheria ambayo taratibu itaenda inaondoa matumizi ya zebaki kutokana na athali yake kwenye kansa hasa ukanda huu wa ziwa ambao umeonekana kasa ni tatizo kubwa ni kweli yamekuwepo malalamiko kuwa maji ya mvua yawezekana yana zebaki lakini mimi nilizungumza na watu wa bonde wakasema wamefanya uchunguzi kila baada ya miezi mi tatu wamedhibitisha kuwa maji yale ni salama, maji yamvua hayana madhara vumbi wanaloliona halina zebaki, zebaki haiwezi kupaa’’ Alisema Constantine Kanyasu Mbunge wa Geita mjini