Home BUSINESS BENKI YA CRDB YAJA NA MUAROBAINI KWA WAJASILIAMARI

BENKI YA CRDB YAJA NA MUAROBAINI KWA WAJASILIAMARI

 
Maafisa wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa wakitoa elimu ya utunzaji wa fedha na kuwafungulia akaunti wanakijiji wa Naunambe wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi.

Na Mwandishi Wetu, Ruangwa | Benki ya CRDB katika kuendeleza juhudi za Serikali katika kuhakikisha wajasiriamali wanafanikiwa katika biashara zao.

Hivi karibuni CRDB imezindua huduma ya utunzaji wa Fedha za wajasiriamali kupitia Akaunti iitwayo Hodari ambayo ni mahususi kwa wafanyabiashara wenye mitaji isiyozidi Milioni 300.

Akiongea na mwandishi wetu Kiongozi wa Mauzo na Huduma za Kibenki wa CRDB Tawi la Ruangwa, Lilian Makawa amesema Akaunti hiyo haina makato ya utunzaji wa fedha wala makato wakati wa kutoa pesa kutoka kwenye Akaunti hiyo.

Hodari Akaunti ni akaunti sahihi kwa Wajasiriamali kwani ni akaunti rahisi kutumia kwasababu ni akaunti isiyo na makato iwe ni wakati wa kutoa hela au makato ya kila mwisho wa mwezi

Mteja wa Akaunti hii ana uwezo wa kutoa pesa zake wakati wowote kwenye ATM, Wakala au ndani ya Benki dirishani,” aliongeza Bi Lilian.

Musa Mpue mmoja wa waendesha Bodaboda katika Kituo cha Mabasi Ruangwa anasema kupitia Akaunti ya Hodari ameweza kuhifadhi makusanyo yake ya kila siku anayoyapata kutokana na biashara yake ya usafirishaji kwa kutumia Bodaboda.

Akaunti ya hodari imenisaidia kuhifadhi makusanyo yangu ya kila siku yatokanayo na biashara yangu ya Bodaboda, na fedha hizo nazipata kwa wakati pale ninapozihitaji kufanya marejesho ya mkopo wangu wa Bodaboda,” alisema Musa.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa na wakati mgumu wanapozitunza pesa zao Benki, pale wanapozihitaji huhitajika kutumia taratibu kadhaa ambazo husababisha kutoweza kufanya miamala ya kibiashara kwa wakati. Benki ya CRDB imeondoa kikwazo hicho kupitia Akaunti hii ya Hodari kwani inawawezesha wafanyabiashara hawa kufanya miamala ya kipesa muda wowote kupitia CRDB Wakala.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here