Kifaa cha kiteknolojia cha kuteketeza taka za hosipitali kilichotengenezwa na TEMDO.
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kufuata miaka 55 ya Azimio la Arusha tasisi ya uhadisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO) imetekeleza Azimio la nchi kutokuwa tegemezi kwa kutegemea nchi nyingine kwa kuhakikisha kuwa Tanzania inajitegemea kiviwanda kwa kutengeneza teknolojia mbalimbali zinazosaidia kupunguza utegemezi.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Mhandisi Profesa Fredrick Kahimba wakati akiongea na waandishi wa habari katika Banda lao lilikuwepo Katika maadhimisho ya miaka 55 ya Azimio la Arusha ambapo alisema kuwa wameijenga hiyo dhana na kusaidia kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa nje ya nchi bidhaa ambazo zinaweza kutengenezewa na watanzania wenyewe.
“Kwa mfano katika sekta ya Afya kwa inaagiza vifaa tiba asilimia 90 na vinavyotengenezwa hapa nchini ni asilimia 10 tu na sisi TEMDO tumeliona hilo na sasa tunatengeneza vifaa tiba ili kuhakikisha kwamba tunapunguza matumizi mengi ya fedha za kigeni zisizo na sababu kwa kuagiza vifaa tiba na kuhakikisha Sasa vifaa hivyo vinatengenezwa hapa nchini kwa bei nafuu na vinawafikia walengwa kwa wakati,”Alisema Mhandisi Profesa Kahimba.
Alifafanua kuwa wameshiriki maonesho hayo yaliyoenda sambamba na maadhimisho kuonuesha uzalendo wao na kuonuesha kuwa bado wanazienzi fikra za Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere za kuhakikisha kuwa wanajenga Tanzania ya ujamaa na kujitegemea ambapo wamekuja kuonuesha teknolojia ambazo taasisi hiyo inaweza kuzitengeneza zikiwa katika sekta mbalimbali.
“Tuna teknolojia ya sekta ya kilimo, afya kama nilivyoelewa awali, sekta ya uvuvi, na zaidi sekta ya viwanda vikunwa na vidogo vidogo kwahiyo tunaunga mkono maadhimisho haya na tutaendelea kuwapa ushirikiano wenzetu wa makumbusho ya Taifa,” Alisema.