Mkurugenzi mtendaji wa shilika la umeme nchini (TANESCO) Maharage Chande amemtaka meneja wa Tanesco mkoa wa Geita kusimamia Vyema mradi wa umeme katika mradi wa umeme kwenye mgodi wa dhahabu wa GGM ambao leo February 21 Tanesco imesai mkataba wa kuuziana umeme na na mdogi huo.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mktaba na mgoodi wa GGM Mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme nchini Maharage Chande amesema mkataba huo utaliwezesha shirika la umeme nchini Tanesco kupata bilioni 5 kwa kila menzi.
Maharage amesema Mkurugenzi wa Tanesco pamoja na viongozi mbali mbali wa Tanesco mkoa wa Geita wanatakiwa kusimamia vyema mradi huo kwani serikali itapata mapato makubwa zaidi kutokana na mapato yatakayo tolewa na mgodi wa dhahabu GGM ambayo yataiwezesha serikali kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
“Sisi sote wafanyakazi wa Tanesco injinia atakae tuangusha hapa lazima turuke naye kwa sababu anatukosesha bilioni 5. Kwa sababu umeme huu utaongeza ufanisi wa kazi zo GGM kwa maana watakuwa wanapunguza gharama katika shughuli zao” Ameaema Maharage Chande mkurugenzi mtendaji shirika la umeme nchini Tanesco.
Makamu wa Rais wa mgodi wa GGM Saimoni Shayo amesema mgodi huo kwa miaka 20 ambayo wamewekeza nchini Tanzania wamekuwa wakitumia umeme wa kazalisha kwa mafuta.
Shayo amesema licha ya umeme wanaotumia mgodini hapo ambao wanazalisha kutokana na mafuta ambayo yanamsamaha wa kodi lakini bado gharama ya kuzalisha umeme ni kubwa kuliko umeme watakao upata kutoka shirika la umeme nchini Tanesco.
“Kwetu hii inamanisha kwamba tunapunguza gharama za uzalishaji kwa maana ya kwamba gharama yetu ya kuzalisha umeme itapungua lakini zaisi tunaangalia matumizi ya kifedha tunapunguza gharama ya mafuta kama tunavyo fahamu dunia sasa inahama kwenye matumizi ya kutumia mafuta ambayoyanazalisha hewa ukaa kwenda kwenye matuzi ya nishati” Amesema Saimon Shayo makamu wa Rais GGM