Home SPORTS CHAMA AAMSHA SHANGWE ZA MASHABIKI WA SIMBA KWA MKAPA

CHAMA AAMSHA SHANGWE ZA MASHABIKI WA SIMBA KWA MKAPA

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM

BAO pekee la kiungo Mzambia, Clatous Chama dakika ya 80 limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 

Sifa zimuendee mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere aliyevunja mtego wa kuotea wa mabeki wa Mbeya Kwanza na kuendeleza shammbulizi lililozaa bao hilo.

Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 31 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tano na watani wa jadi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.

Mbeya Kwanza wanabaki na pointi zao 13 za mechi 14 pia katika nafasi ya 12.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here