Home BUSINESS WANANCHI WAIOMBA BRELA KUONGEZA MUDA KATIKA KAMBI YAO JIJINI DAR

WANANCHI WAIOMBA BRELA KUONGEZA MUDA KATIKA KAMBI YAO JIJINI DAR


Na: Hughes Dugilo, DAR.

Makundi ya watu mbalimbali wameendelea kupatiwa Elimu inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA Katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Katika siku ya nne ya zoezi hilo Januari 29,2022 kulionekana watu wengi wakiendelea kupatiwa huduma Viwanjani hapo huku baadhi yao wakiomba kuongezwa muda wa zoezi hilo.

Katika mahojiano maalum na waandishi wa habari viwanjani hapo Afisa msaidizi wa Usajili wa BRELA Vyonne Maselle ameeleza kuwa kumekupo na muamko mkubwa kwa wananchi kutaka kusajili Biashara zao na kwamba wao kama BRELA wameweka mikakati ya kuhakikisha wafanyabishara wanarasimisha biashara zao.

“Lengo letu tunataka wafanyabiashara wawe wamekamilika, wamesajili kampuni, wamepata leseni na wamerasimisha biashara zao.” ameeleza.

Aidha ametoa mwito kwa wananchi kufika katika maeneo hayo ili waweze kuhudumiwa ikiwa pamoja na kusajili majina ya biashara na kampuni ikiwa imesalia siku moja zoezi hilo kufika tamati.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here