SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limetangaza rasmi kuanza mgao wa umeme wa siku 12 nchi nzima kuruhusu matengenezo ya mitambo ya kufua umeme kote nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Maharage Chande ametanganza leo Ijumaa Jan. 28 kuwa mgao huo utaanza Jumamosi, Januari 29 hadi Februari 10 mwaka huu.
Taarifa na ratiba ya mgao huo itatolewa kuruhusu watanzania na taasisi kupanga ratiba zao.
Kwa mujibu wa Tanesco maboresho katika mtambo wa kufua umeme wa Kinyerezi I na Ubungo III yataongeza uzalishaji kutoka megawati 150 hadi megawati 335.