Home SPORTS MUKOKO TONOMBE ATIMKIA TP MAZEMBE

MUKOKO TONOMBE ATIMKIA TP MAZEMBE


KIUNGO Tonombe Mukoko ameachana na klabu ya Yanga na kujiunga na TP Mazembe ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Taarifa ya Yanga jioni hii imemshukuru Mukoko kwa mchango wake kama Nahodha Msaidizi kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu tangu awasili kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa.

Mukoko anakwenda Mazembe wiki moja baada ya Yanga kumsajili Mkongo mwingine, winga Chico Ushindi kutoka klabu hiyo ya Lubumbashi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here