Home LOCAL GEITA YAJIPANGA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 286 MAPATO YA NDANI.

GEITA YAJIPANGA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 286 MAPATO YA NDANI.

Na: Costantine James Geita.

Mkuu wa mkoa wa Geita mhe. Rosemary Senyamule amezitaka halmashauri ndani ya Mkoa huo kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato pamoja na ulipaji wa kodi ili kuweza kufikia kasi ambacho halmashauri hizo zimejipangia kukusanya  kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Leo januari 28, 2022 Kamati ya Ushauri Mkoa wa Geita (RCC) imeketi ili kujadili na kupitisha Makisio na mapendekezo ya Bajeti ya Mkoa wa Geita pamoja na Halmashauri zake ambapo jumla ya Tshs bilioni. 286.574 zitatumika huku Halmashauri zikikisia kukusanya jumla ya Tshs bilioni. 27 .373, kutoka kwenye vyanzo vya ndani.

Katika Kikao cha RCC kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita, mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule ameziagiza Halmashauri ndani ya mkoa huo kuongeza ubunifu  katika nyanja za kukusanya mapato na kuhamasisha ulipaji wa kodi kwenye maeneo yao ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri.  

“Tumejiongezea kidogo kipimo cha mapato ya ndani kutoka bilioni 25, mwaka ujao wa fedha tunataka tukusanye bilioni 27  tumejiongezea bilioni mbili, Niendelee kusisitiza ukusanyaji wa mapato na ulipaji wa kodi ambazo tumeziona hasa kwenye mapato ya ndani ya halmashauri mpaka disemba tumefikia asilimia 53% bado asilimia 57% katika miezi sita tukazane kukusanya mapato hayo kwa uaminifu mkubwa ili tuweze kufikia lengo kwa sababu kubwa yakuweza kuapata uwezo wa kuwahudumia wananchi wetu “Rosemary Senyamule mkuu wa mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wazazi wote mkoa wa Geita ambao wanawajibu wa kuwapeleka watoto shule kwenda kujiandikisha kufanya hivyo ili watoto hao waanze kupata elimu kama serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassani ilivyo zamilia  kutoa elimu bure kwa kujenga miuondombinu bora  ya shule ili kuondokana na kero ya ukosefu wa madarasa.

“Hali ya kuripoti shuleni kwa shule za msingi ni nzuri sana ila kwenye shule za Sekondari tunataka tufikie malengo ya watoto kuripoti kwa zaidi ya wanafunzi laki moja na arobaini na moja kama tulivyokusudia hivyo tukahimizane wazazi wapeleke watoto shuleni.” Amesema Mhe. Rosemary Senyamule mkuu wa mkoa wa Geita.

Mhe. Dkt. Medard Kalemani Mbunge wa Chato katika kikao hicho ameshauri pamoja na uwepo wa ujenzi wa vituo vya afya kwenye tarafa pia vijengwe vituo vya afya kwenye kata zilizo mbali na makao makuu ya tarafa ili kuondoa kero ya ukosefu wa huduma za afya kalibu na wananchi.

 “Ukitazama kitarafa utakuta kila tarafa inakituo cha afya lakini unakuta tarafa moja inakata nyingine zipo mbali mbali na unakuta tarafa moja ipo mbali takiribani zaidi ya  kilomita 30 kutoka kwenye kituo cha afya kimoja ndani ya tarafa hiyo, kwahiyo ushauri wangu mhe. Mwenyekiti labda liwekwe vizuri kimpango pamoja na kujenga vituo cha afya kwenye tarafa  lakini tujielekeze pia sipesifikale kwahizo kata ambazo ziko mbali  sana na kituo cha afya kwenye tarafa” Amesema Mhe. Dkt. Medard Kalemani Mbunge wa Chato.

Kwa upande wake Mbunge wa Geita mjini ameomba katika bajeti hiyo kuboresha miundombinu ya barabara hasa barabara ya Geita-Kahama kwani barabara hiyo inatumiwa na wananchi wengi katika shughuli mbali mbali za kiuchumi.

 “Niombe tu mhe. Mkuu wa mkoa wakati ukifikisha salamu zetu kwa mhe rasi  basi umhimu mkubwa wa barabara hii  ni kwamba Migodi yote mikubwa  nchi hii miwili inaitegemea barabara hii ndani ya mkoa huu inaunganishwa na Barabara ya Geita-Kahama, barabara hii inabeba mizigo mikubwa sana hivyo inapasa kuboreshwa kuwa ya kiwango cha lami ili itumike na kudumu kwa muda mrefu”, amesema Mhe. Constantine Kanyasu, Mbunge wa Geita Mjini. 

Mbunge wa Nyang’hwale Mhe. Hussein Nassor na Makamu Mwenyekiti wa Nyang’hwale wamelalamikia kuchelewa kwa kukamilika  ujenzi wa jengo la Halamshauri hiyo huku wakitoa  rai kwa Serikali kuwaangalia kwa jicho la huruma ili wapate mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami na kuchepusha barabara ili kutatua kero ya wanafunzi kugongwa na magari kutokana na barabara kukatisha kwenye shule ya Sekondari ya Nyang’hwale. 

“kuna baadhi ya mambo ambayo tumeshauri ikiwemo barabara inayopita pale  sekondari  ya nyang’hwale nyang’hwale sekondari pale ile shule barabara limepita katikati hilo  barabara ni hatali kwa wanafunzi, watumishi lakini pia kwa wanao tumia barabara hilo ni hatali sana kwa maisha yao kwa sababu magari yanapita pale kwa mwendo kasi tumeshauri kwamba barabara lile liweze kuchepushwa angalau kuepusha hizo ajali. Amesema Mhe. Hussein Nassor mbunge wa Nyang’hwale. 

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here