Home BUSINESS BRELA YATANGAZA KUONGEZA MUDA WA UTOAJI ELIMU NA HUDUMA JIJINI DAR

BRELA YATANGAZA KUONGEZA MUDA WA UTOAJI ELIMU NA HUDUMA JIJINI DAR

DAR ES SALAAM.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetangaza kuongeza muda wa utoaji Elimu na Huduma katika eneo la Mlimani City Jijini Dar es Salaam hadi siku ya jumatano Februari 2, 2022.


Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano BRELA inasema kuwa hatua hiyo imetokana na wadau wengi kujitokeza kwa wingi kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa na BRELA katika muda wa siku tano zilizopangwa awali hivyo kulazimu kuongeza muda wa siku tatu ili kuendelea kutoa Huduma kwa ufanisi zaidi.


BRELA inawahimiza wananchi kufika katika viwanja vya Mlimani City ili kupata Elimu na  Huduma mbalimbali inazotoa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here