Home SPORTS AZAM YATINGA HATUA YA 16 YA (ASFC), YAICHAPA TRANSIT CAMP 1-0

AZAM YATINGA HATUA YA 16 YA (ASFC), YAICHAPA TRANSIT CAMP 1-0

Na: Stella kessy, DAR.

KIKOSI cha Azam kimetinga hatua ya  16 ya michuano ya Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa Transit Camp bao 1-0 katika Uwanja wa Azam Complex , nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Huku bao pekee la Azam limefungwa na nahodha, beki mkongwe Aggrey Morris dakika ya 30 hata hivyo kwa ushindi huo, Azam FC inakwenda Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ambako itamenyana na Baga Friends. 

Mechi nyingine za leo za Azam Sports Federation Cup, Namungo FC imeitoa Lindi United kwa kuichapa 2-0 Uwanja wa Ilulu mjini Lindi na Pamba FC imeitoa Stand United kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mabao yote ya Namungo leo yamefungwa kwa penalti na Shiza Kichuya na Ibrahim Mkoko, wakati ya Pamba yamefungwa na Willy Magai na Moses Msukanywele .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here