Home BUSINESS RC MAKALLA: UKARABATI NA UJENZI SOKO JIPYA KARIAKOO KUANZA WIKI IJAYO.

RC MAKALLA: UKARABATI NA UJENZI SOKO JIPYA KARIAKOO KUANZA WIKI IJAYO.


 
– Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha Biloni 28 na kuwajali Wafanyabiashara

– Asema Wahanga wa soko la Kariakoo Na soko Dogo watapewa kipaumbele kurejea soko litakapokamilika.

– Asema Mkandarasi wa kukarabati Na kujenga soko amepatikana.

Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Ukarabati wa Soko la Kariakoo lililoungua na  Ujenzi wa Soko jipya la Gorofa 6 utaanza Baada ya Tar 09 Disemba baada ya Mkandarasi kupatikana.

RC Makalla amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Shilingi bilioni 2 kwa vikundi vya ujasiriamali ambapo amesema tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi Cha Shilingi bilioni 28 kwaajili ya Ujenzi huo.

Aidha RC Makalla amewaondoa hofu Wafanyabiashara wa Soko Hilo Wenye wasiwasi kuwa baada ya ujezi kukamilika watapangishwa watu wengine ambapo amesema wazawa watapewa kipaombele.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here