Home LOCAL LUBINGA AKUTANA NA UONGOZI WA TAWI LA CHUO KIKUU KAMPALA

LUBINGA AKUTANA NA UONGOZI WA TAWI LA CHUO KIKUU KAMPALA


Katibu wa NEC- Siasa na uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiongea na Uongozi wa Tawi la UVCCM Chuo Kikuu cha Kamapala ambao ulimtembelea ofisini kwake Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam.


Katibu wa NEC- Siasa na uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Tawi la UVCCM Ndugu Hakim Steven Bright kiasi cha shilingi 450,000/- kwa ajili ya uboreshaji wa ofisi yao.Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Picha na CCM Makamo Makuu

Katibu wa NEC- Siasa na uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga leo amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Tawi la UVCCM Chuo Kikuu cha Kamapala ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Hakim Steven Bright katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam.


Pamoja na mambo mengine Katibu wa NEC-Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ameukabidhi Uongozi huo kiasi cha fedha 450,000/- ikiwa sehemu ya fedha walizoomba kukamilisha uboreshaji wa ofisi yao iliyopo katika Tawi la Kilimo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here