Home SPORTS KIDUNDA, KATOMPA NGOMA DROO

KIDUNDA, KATOMPA NGOMA DROO


Na: Stella Kessy, DAR

PAMBANO la kugombani mkanda kati ya  Suleiman Kidunda na Erick Tshimanga Katompa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) liliishia Raundi ya tatu baada ya wawili hao kugongana vichwa na ukumbi wa Ubungo wa Plazza Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Hata hivyo kwa kutumia  sheria za WBF baada ya bondia Mtanzania, Kidunda kuchanika juu ya jcho kufuatia kugongwa kichwa na Katompa mwanzoni mwa Raundi ya nne, majaji waliamua kutoa droo.

Lakini pia majaji waliweka wazi hadi pambano hilo la uzito wa Middle kuwania ubingwa wa Mabara wa WBF, Kdunda alikuwa anaongoza kwa pointi.

Ikumbukwe, Katompa alimtwanga kwa KO Mtanzania mwingine, Abdallah Shaabani Pazi ‘Dullah Mbabe’ Oktoba 9 mwaka jana ukumbi wa PTA, Temeke JijininDar es Salaam na jana Kidunda alipewa nafasi kubwa ya kumlipia kisasi Mtanzania mwenzake. 

Katika mapambano mengine ya jana Mtanzania, Ismail Galiatano alishinda kwa pointi dhidi ya Denis Mwale wa Malawi kwenye pambano la nane na kutwaa taji la P.S.T uzito wa Super Bantam.  

Mtanzania, mwingine, George Bonabucha alimshinda kwa pointi Mzimbabwe, Hassan Milanzi kwenye na kutwaa pia mkanda wa P.S.T, wakati Grace Mwakamele alikuwa Mtanzania pekee aliyepoteza pambano usiku huo baada ya kushindwa kwa pointi na Mmalawi, Ruth Chisale aliyejinyakulia taji la PST pia.          Oscar Richard pia alibeba mkanda wa PST baada ya kumtwanga Paul Magesta, Ibrahim CMgendera ‘Ibrah Class alikalisha Kelvin Majiba kwa Knockout (KO).

Juma Choki alimkalisha kwa KO, Salim Chazama, Vigulo Shafi akamshinda kwa pointi Ally Kilongola  na Mwanajeshi mwingine, Haruna Swanga akameshinda Daniel Matefu kwa KO kwenye pambano la tano usiku huu lenye raundi nne.

Iddi Jumanne alimchapa Hamis Kibodi kwa pointi , Joseph Mchapeni alimkalisha Paschal Goba kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya raundi ya pili, Najma Isike akashinda kwa pointi dhidi ya Leila Yazidu na King Makassy alimshinda kwa pointi Ibrahim Mpili.

Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TATU DISEMBA 27-2021
Next articleACEX CEO URGES LOCAL INVESTORS TO USE DIGITAL PLATFORM IN TRADING EFFECTIVELY
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here