Home SPORTS YANGA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA MBEYA KWANZA KESHO

YANGA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA MBEYA KWANZA KESHO

Na: Mwandi wetu, MBEYA.

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kuelekea katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Mbeya Kwanza  wanachohitaji ni ushindi na sio kingine katika  mchezo huo.

katika mchezo uliopita Yanga walitoka sare dhidi ya Namungo kwa bao 1-1, mchezo uliopigwa katika dimba la Ilulu Mjini Lindi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kikosi kimejipanga kupata matokeo kesho  na kutaka wadau na mashabiki kusahau mchezo wao dhidi ya Namungo ambao tangu ligi kuanza ni mara ya kwanza kutoka sare jambo ambalo lilikuwa sio malengo ya klabu yao. 

“Mchezo uliopita tulitoka sare na Namungo, mchezo wa kesho tunacheza  na Mbeya Kwanza tukiwa ugenini, hatuhitaji jambo lingine zaidi ya ushindi, Wanayanga wote pia hawahitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi na ndio maana tunawaambia kuwa Mbeya Kwanza watatusamehe”amesema.

Ameongeza kuwa kwa sasa ligi imekuwa ngumu lakini hakuna jambo ambalo linawazuia kupata ushindi  kwani kikosi kimejiangaa kutwaa ubingwa kwa msimu huu .

Kikosi cha yanga kimetua Mbeya Novemba 28  kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa ligi unaatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here