Home SPORTS UCHAGUZI KIKAPU KUFANYIKA DISEMBA 30 MWAKA HUU

UCHAGUZI KIKAPU KUFANYIKA DISEMBA 30 MWAKA HUU



Na: Stella kessy

BARAZA la michezo la Taifa (BMT) limewatangaza wadau wa michezo ya mpira wa kikapu kuwa kutakuwa na uchaguzi wa viongozi  utakaofanyika Disemba 30 mwaka huu jijini Dodoma.

Akizungumza leo na waandishi wa habari leo  Kaimu Mkuu wa kitendo cha Uhusiano Najaha Bakari amesema kuwa fomu hizo zinaanza kutolewa na kurudishwa kuanzia leo 25 Novemba  na mwisho wa kuchukua fomu ni Disemba 24.

Fomu hizo zinatolewa katika ofisi za BMT zilizopo uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo usajili wa viongozi watajiongeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, utakaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Disemba 2021.

Alitaja nafasi zinazogombewa ni pamoja na Rais,Makamu wa Rais,Katibu Mkuu,Katibu Mkuu msaidizi,Mwema hazina ambao ada  yao ni shilingi  500,000 ,wakati Kamishina wa mipango na maendeleo,Kamishina wa Makocha,Kamishina wa Ufundi na uendeshaji mashindano,Kamishina ya Uamuzi.

Nafasi nyingine Kamishina wa watoto wadogo na Maendeleo ya shule,Kamishina ya wanawake, watu wenye Ulemavu’ na tiba  ya wanamichezo  ambao watalipa ada ya shilingi 200,000.

Katika uchaguzi huo mgombea anatakiwa kuwa  na sifa zifuatazo,awe raia wa Tanzania na umri usiopungua miaka 25, huku katika nafasi ya makamu wa rais mgombea natakiwa kuwa na umri wa miaka kuanzia 30. 

Ameongeza kuwa kwa upande wa elimu anatakiwa awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea,pia awe na uzoefu wa kitaifa na wa kimataifa juu ya nafasi ya uongozi anayogombea.

Pia awe na uwezo wa kuandika na kusoma kingereza na kiswahili,pia awe na akili timamu na hajawahi kuugua ugonjwa wa Akili, awe hana makosa ya ya kijinai, pia anatakiwa ambaye alishawahi kuwa mchezaji  wa mpira wa kikapu au kuhuzuria mafunzo ya ualimu wa mpira wa kikapu,uamuzi ,utawala wa michezo,tiba ya wananichezo au utunzaji na utengenezaji wa viwanja vya michezo.

Hata hivyo malipo ya fomu yafanyike katika akaunti ya Baraza kwa kutumia mfumo mpya wa malipo ya Serikali.

Aidha risiti ya malipo iwasilishwe baraza pamoja na fomu zilizojazwa kwa umakini na usahihi na kuambatanisha na nakala za nyaraka zote kulingana na sifa mahususi zilizoainishwa katika katiba ya chama hiki.

Hata hivyo baraza limetoa wito kwa wote wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi huo na maendeleo ya michezo nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here