Home LOCAL TMDA YATOA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA MWAKA MMOJA WA MRADI WA ASCEND

TMDA YATOA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA MWAKA MMOJA WA MRADI WA ASCEND

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) Bw. Adam Fimbo akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Mradi wa ASCEND mapema jana Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa muda wa mkutano wa mwaka wa Mradi wa ASCEND, Prof. Blandina Mmbaga akizungumzia mkutano huo kwa Waandishi wa habari (Hawapo pichani).

Mshiriki kutoka Zanzibar ambaye ni mtafiti akizungumza katika mkutano huo.

DAR ES SALAAM.

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa kushirikiana na wadau wakiwemo watafiti, imekutana kupitia na kutoa tathimini ya utekelezaji wa mwaka mmoja wa mradi wake wa ASCEND  unaolenga kuboresha mifumo ya udhibiti wa majaribio ya Dawa na tafiti mbalimbali nchini.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa mwaka wa mradi wa ASCEND, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo alisema kuwa, kupitia mradi huo wameweza kupokea fedha ambazo zimewasaidia kutoa miongozo kwa watafiti wanaofanya kwenye majaribio ya dawa, wanyama ilikunda afya za wananchi kupitia kwenye majaribio hayo.

“Wale wote wanaotaka kufanya utafiti, lazima wafuate taratibu zilizowekwa. Sekta ya dawa huwezi kufanya utafiti pasipo majaribio, dawa inaanza kufanyika kwa wanyama na baadae kwa binadamu hivyo tunatakiwa kudhibiti mapema na kumtaka mtafiti kufuata miongozo ya kitalaamu ambayo tunaitoa sisi.

“Kazi kubwa tunayoifanya kila siku ni kudhibiti hayo majaribio, kufuatilia hali ya usalama kwa dawa zinazotolewa kwa binadamu kama zinadhuru ama hadhidhuru watu”. Alisem Adam Fimbo.

Aidha, alisema kuwa, TMDA wamekuwa wakipokea maombi ya kufanya majaribio ya utafiti kati ya 20 hadi 30 kila mwaka ambapo wanayakagua na kisha kutoa vibali, lengo ni kulinda watanzania wanaoshiriki kwenye hayo majaribio.

“Hatuwezi kuruhusu watu kufanya majaribio ya dawa pasipokupitia kwenye maabara zetu.

Majaribio mengi yanafanyika kwenye chanjo, magonjwa ya Malaria, Kifua kikuu [TB], na magonjwa mengine ambapo yanahusisha binadamu na wanyama pia.” alisema Bw. Adam Fimbo.

Aidha, ameongeza kuwa, mwezi huu wameweza kukamilisha mwaka mmoja kamili tangu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo wa ASCEND  tokea uanze rasmi Novemba 26  mwaka jana.

“Muda muafa kukutana na kujadili namna mradi unavyoenda na nini cha kufanya katika kujadili kwa pamoja na kuja na matokeo chanya huku tunaingia mwaka wa pili kwa utekelezaji wa mradi huu na tumebakiza miezi 15 tu mradi huu kuisha rasmi hapo Apri 30 mwaka 2023.

Kikubwa ni kuangalia tumetekeleza nini, tumebakiza nini kwenda mbele na mengine iliwaliotupatia fedha za mradi wajue tulichotekeleza.”  alisema Bw. Adam Fimbo.

Aidha, Bw. Adam Fimbo alisema kuwa, TMDA wanawajibu pia kuweka mifumo ya udhibiti wa dawa kama sheria ya utekelezaji wa dawa na vifaa tiba sura ya 2019, hivyo kupitia mradi huo wa ASCEND umeweza kuendeleza ujengwaji wa mifumo imara na thabiti ya tafiti na kisheria.

“Tumeweka miongozo na mifumo kwa wale wote wanaotaka kutafiti kwenye majaribio ya dawa lazima tuwaruhusu na mradi huu ndo uliwezesha namna ya kujijenga katika kufikia shughuli hizo za majaribio.” Alisema Adam Fimbo.

Amesema wataweka mifumo vizuri ya kufuatilia wale ambao watapata madhara wakati wanatumia Dawa za majaribio kwa kutokujua Kama ni salama au si salama na kuhakikisha wale wanaotumia Dawa hizo wanabaki salama.

Kwa upande wake, Meneja Mipango wa mradi huo wa ASCEND, Bi. Kissa Mwamwita amesema mradi huo utasaidia kuboresha ufanisi na ubora wa kazi ya Wakala  wa Kitaifa wa maadili ya utafiti na udhibiti kwa ukaguzi wa majaribio ya Kiliniki na uangalifu wa dawa.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here