Home SPORTS TANZANIA YACHAPWA 1-0 NA UGANDA Canaf

TANZANIA YACHAPWA 1-0 NA UGANDA Canaf

Na: Stella Kessy,  DAR ES SALAAM

TIMU  ya Uganda  leo imeibuka na ushindi dhidi ya  Tanzania kwa bao 1-0 katika  mashindano yanayoendelea  ya Afrika  soka  kwa wenye ulemavu CANAF 2021 katika  Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika dakika 20 mshambuliaji Ssempija Julius wa Uganda  aliipatia timu yake bao ambalo lilidumu dakika zote za mchezo.

Katika mchezo wa kwanza Tanzania iliibamiza timu ya Morocco 2-1. Wakati Uganda katika mchezo wake na Sierra Leone walifungwa 3-0.

Mchezo huu umechezeshwa na  Luciano Antonio kutoka Angola, Mohamed Mwadini kutoka Zanzibar na David Mng’ong’o kutoka Tanzania.

Mechi nyingine kati ya  Morroco imeibuka na ushindi wa bao 3-0 

Huku  bao yote yamefungwa na Redouane Chaanoun  huku mchezo mwingine ukiwa kati ya Kenya na Zanzibar, Liberia na Gambia pia Nigeria na Misri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here