– Asema Ujenzi wa Vibanda vya kisasa upo hatua ya mwisho kukamilika.
– Awalika wananchi kufika coco beach kupata huduma ya vyakula Na burudani.
– Asisitiza ulinzi na usalama wa WANANCHI Na usafi kuzingatiwa kwenye eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Alhamis ya November 04 anatarajia kuambatana na moja ya Kiongozi kuelekea ufukwe wa Coco ili kumuonyesha maboresho makubwa yaliyofanyika.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea fukwe hiyo na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Vibanda vya kisasa ambapo ameonyesha kufurahishwa na Mapinduzi makubwa yaliyofanyika kwenye ufukwe huo na kuwahimiza Wadau kukamilisha Ujenzi mapema.
Aidha RC Makalla amesema kukamilika kwa ufukwe huo kutachochea ukuaji wa utalii wa fukwe na kuchochea shughuli za Biashara Jambo litakalosaidia Wafanyabiashara kupata kipato na Serikali kupata Kodi.
Miongoni mwa maboresho makubwa yanayofanyika kwenye ufukwe huo maarufu kwa uuzaji wa mihogo ni pamoja na Ujenzi wa Vibanda vya kisasa, Ujenzi wa migahawa ya chakula, Ujenzi wa vyoo, Usafi wa mazingira, matamasha makubwa ya Burudani, Umeme, Maji, sehemu za huduma za Kifedha na Mambo mengineyo ikiwa ni juhudi binafsi za RC Makalla kutafuta Wadau waliojitolea kuwajengea Vibanda vya kisasa bure Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya Biashara eneo Hilo.