Home LOCAL RC MAKALLA AITAKA TMDA KUDHIBITI WIZI WA DAWA NA DAWA BANDIA.

RC MAKALLA AITAKA TMDA KUDHIBITI WIZI WA DAWA NA DAWA BANDIA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla akizungumza wakati wa tukio hilo la mafunzo ya siku tano kwa wakaguzi wa dawa wa Manispaa wa Mkoa wa huo.
 

– Awataka Kudhibiti wizi wa Dawa za Serikali na kutokomeza Dawa Bandia.

– Asisitiza kufanyika kwa ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kudhibiti wezi wa dawa Na  dawa bandia.

– Ataka “vishoka” ambao ni wakaguzi feki kukomeshwa.

DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameielekeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA kupatia ufumbuzi tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali na kutoa onyo kwa Maduka yanayonunua dawa za Wizi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Mafunzo ya siku tano kwa Wakaguzi wa Dawa wa Manispaa za Mkoa huo yaliyolenga kuwajengea uelewa wa maadili ya kazi na utambuzi wa dawa Bandia ili kuongeza ufanisi kwa faida ya watumiaji wa dawa.

Aidha RC Makalla amewataka Wakaguzi wa Dawa kuzingatia Weledi na maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo Kutokana na unyeji wa kazi hiyo ambayo inabeba dhamana ya Maisha na uhai wa Wananchi.

Hata hivyo RC Makalla ametaka Mamlaka hiyo Kudhibiti tatizo la Vishoka Wanaofanya ziara za ukaguzi kwenye Maduka huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa Maduka ya dawa.

Pamoja na hayo RC Makalla ameitaka Mamlaka hiyo kuweka utaratibu wa kufanya ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kubaini wababaishaji na kutaka uwepo wa watoa huduma Wenye sifa na Vigezo.

Video


 

Previous articleRC SINGIDA AKABIDHI BASI HOSPITALI YA MANDEWA KWA AJILI YA KUSAFIRISHIA WAFANYAKAZI
Next articleHABARI ZILIZOPO MAGAZETI YA LEO J.TANO DISEMBA 1-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here