Home LOCAL RAIS SAMIA NA RAIS MUSEVEN WAZINDUA SHULE YA AWALI MSINGI CHATO

RAIS SAMIA NA RAIS MUSEVEN WAZINDUA SHULE YA AWALI MSINGI CHATO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa pamoja wakiondoa kitambaa  kuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi Museveni Pre & Primary School  iliyojengwa kwa msaada wa Rais  Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi Museveni Pre & Primary School iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita.


Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akimkabidhi mfano wa funguo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kama ishara ya makabidhiano ya Shule hiyo ya Awali mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika Shule hiyo ya Museveni Pre & Primary School Chato mkoani Geita


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakikagua baadhi ya majengo ya Shule hiyo ya Awali na Msingi iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Chato mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021 mara baada ya kuizindua rasmi Shule hiyo.

  Muonekano wa  majengo ya Shule ya Awali na Msingi iliyojengwa kwa msaada wa  Rais Yoweri Museveni Chato mkoani Geita.

PICHA NA IKULU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here