Home LOCAL MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA BONAH AMPONGEZA RAIS SAMIA

MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA BONAH AMPONGEZA RAIS SAMIA

 

NA: HERI SHAABAN

MBUNGE wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Hassan  Suluhu,kwa kuipatia jimbo la Segerea Bilioni 1.6 kwa ajili ya madarasa ya UVIKO 19

Mbunge Bonah alitoa pongeza hizo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakati wa ziara yake ya Sekta ya Elimu kukagua madarasa ya elimu sekondari.

“Nampongeza Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani jimbo langu la Segerea  nimepewa shilingi Bilioni 1,620,000,000 kwa ajili ya msdarasa ya UVIKO   wanafunzi wetu waje kusoma ” alisema Bonah 

Mbunge Bonah  alisema Taifa lolote ili liweze kuendelea lazima watu wake wasome  atasimamia madarasa hayo kila kata na madiwani wa kata zote kuakikisha madarasa yanaisha kwa wakati.

Katika ziara hiyo Mbunge Bonah alitembelea Kata ya Kinyelezi ,Kimanga na Bonyokwa katika kata ya Kinyelezi mbunge Bonah alitoa ahadi ya Fedha za Mfuko wa Jimbo kujenga vyoo vya Walimu sekondari ya kinyelezi mpya yenye changamoto ya vyoo .

Diwani wa Kinyelezi Leah Ngitu   alisema  kata ya kinyelezi wamepewa milioni 200  kwa ajili ya kituo cha afya cha kata hiyo .

Leah alimpongeza Mbunge Bonah kutatua changamoto za kata hiyo kwa fedha za Mfuko wa jimbo .

Diwani wa Bonyokwa Tumike Malilo  alimpongeza Mbunge kwa kuwavutia umeme sekondari ya Bonyokwa ambapo kwa sasa wanafunzi wanasoma katika mangira bora na salama .

Diwani tumike alisema mikakati yake Kata ya Boyokwa wanafunzi wasome kidato cha tano na kidato cha sita ambapo alimshauri mbunge ili kurahisisha wanafunzi shule za kata wasome karibu

Mwisho

Previous articleKMC KUWAFUATA MBEYA CITY KIBABE
Next articleREA YAMWAHIDI MATOKEO CHANYA MKUU WA MKOA WA RUVUMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here