MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamemtambulisha Mspaniola, Pablo Franco Martín kuwa kocha wao mpya Mkuu anayechukua nafasi ya Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa aliyefukuzwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Pablo aliyezaliwa Juni 11 mwaka ni kocha mwenye uzoefu aliyefundisha klabu mbalimbali nchini kwao, ikiwemo mabingwa wa kihistoria wa Ulaya, Real Madrid.
Pablo mwenye umri wa miaka 41, mzaliwa wa Madrid, alianza kufundisha Coria mwaka 2008 hadi 2009 akaenda Fuenlabrada kote kama Kocha Msaidizi.
Mwaka 2010 alikuwa Kocha Mkuu wa Santa Eugenia hadi 2012 Illescas akahamia Puertollano hadi 2014 akaenda Getafe B hadi 2015 Getafe A katika La Liga hadi 2016 akahamia Saburtalo Tbilisi ya Georgia hadi 2017.
Kutoka hapo akatua BSU ya China hadi akarejea Hispania na kuwa Kocha Maaidizi wa Real Madrid hadi 2019 alipojiunga na Al-Qadsia ya Kuwait hadi anahamia Simba SC mwezi huu.