Home BUSINESS HALMASHAURI YA KALIUA YATOA MIL 240 MIKOPO YA ASILIMIA 10

HALMASHAURI YA KALIUA YATOA MIL 240 MIKOPO YA ASILIMIA 10

Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batrida Buriani (katikati) akikata utepe na kuwakabidhi watendaji na wasiliamali pikipiki hizo kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Kaliua Paul Matiko Chacha.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batrida Buriani akiwa ameshilia mfano wa hundi kwa ajili ya kuwapatia wajasiliamali wa wilaya ya kaliua mkoani Tabora jana.

Mjasiliamali wa vikundi vya Madinda Pure Honey, Paul Madinda Akiwa katika biashara yake ya asali.

Na: Lucas Raphael,TABORA

Halmashauri ya wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora ,imetoa kiasi cha shilingi milioni 240 ya  asilimia 10 kwa  ajili ya mkopo kwa wanawake ,vijana na walemavu  

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo  Jerry Mwanga alitoa kauli hiyo kwenye uzinduzi wa soko la mazao ya nyuki ,utoaji mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali na kukabidhi pikipiki kwa watendaji wa kata katika ukumbi wa Flangenge wilayani humo.

Alisema fedha zilizotolewa na halmashauri ya kaliua zinawawezesha wanawake ,vijana na walemavu kiuchumi katika wilaya hiyo ,ambapo inavikundi 826 vyenye wanachama 8,820.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba kutokana na ufinyu wa fedha zinazopatikana katika halmashauri ina uwezo wa kutoa mikopo kwa vikundi 45 vya wajasiliamali   .

Aidha mkurugenzi huyo alibainisha kwamba kwa upande wa kuwawezesha vikundi vya vijana halmashuari ina uwezo wa kutoa fedha za mikopo kwa  vikundi 33 kati ya vikundi 128 kwa mwaka sawa na asilimia 35 na walemavu vikundi 10 kwa mwaka kati ya mahitaji ya vikundi 20 sawa na asilimia 2.

Jerry alisema kwamba katika sekta ya maendeleo ya jamii ambayo ikitumika vizuri inaweza kuleta mabadiliko chanja na kwa haraka kwa jamii nzima.

Wakati huohuo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo alitoa pikipiki 40 kwa wajasiliamali 15 na watendaji kata 35 zenye thamani ya shilingi  zaidi ya million 69 kwa ajili waweze kufanyakazi zao vizuri.

Hata hivyo alisema halmashauri hiyo katika jitihada   mikakati zaidi inahitajika ili kuwa na uwezo wa kukopesha vikundi vingi ilikupunguza tatizo la ajira na kuwainua kiuchumi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Batrida Buriani aliwataka wajasiliamali wote waliopata fedha za mkopo kutoka katika halmashauri hiyo wawahi kurejesha kwa kufuata maelekezo waliopewa ili na watu wengine wenye sifa waweze kupatiwa ili kutekeleza agizo la Rais.

Balozi huyo alisema ili kuwa mwaminifu katika serikali yetu hasa inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasani kwa mujibu wa sheria warejeshe harasa marejesho yao bila kufuatiliwa na halmashauri na kufikishwa mahakamani.

Alisema wajasiliamali wadogo wote waliopata fedha za mkopo na makatibu kata waliopata pikipiki hizo wafuate sheria na maelekezo waliopewa na sio kukiuka watapoteza sifa za kuaminiwa na serikali.

Nao Mjasiliamali wa vikundi vya Madinda Pure Honey, Paul Madinda ambaye anajishughulisha na uuza asali  ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia mikopo hiyo ambayo itawasaidia kuinuka uchumi  .

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here