Home LOCAL BALOZI WA UFARANSA NABIL HAJLAOUI, MABALOZI WA EU, NA WADAU KUSHIRIKIANA NA...

BALOZI WA UFARANSA NABIL HAJLAOUI, MABALOZI WA EU, NA WADAU KUSHIRIKIANA NA RAIS SAMIA KUPINGA UKATILI WA KUJINSIA

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya wakizungumzia siku 16 za kupinga ukatili wa ukatili wa kijinsia hapa nchini uliofanyika kwenye kituo cha utamaduni cha ufaransa Jijini Dar es Salaam. ( wa kwanza kulia) ni, Balozi wa Irelend nchini Tanzani Ms Mary O’Neill , (kushoto) ni Balozi wa umoja wa Ulaya Manfredo Fanti.
 
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano .
 
Balozi wa umoja wa Ulaya Manfredo Fanti akitoa taarifa ya pamoja ikiwakilisha umoja huo kuhusu siku 16 za ukatili wa kijinsia.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Nørgaard Dissing-Spandet (kulia) akizungumza kwenye mkutano huo Jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa kutoka Ubalozi wa Ujerumani Dkt.
Dr. Katrin Bornemann akizungumza kwenye mkutano huo.

Balozi wa Irelend nchini Tanzani Ms Mary O’Neill ,akizungumza kwenye mkutano huo


Mwakilishi kutoka ubalozi wa Uholanzi Bw.
Job Runhaar akizungumza na waandishi wa habari

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UN Women  Hodan Adou akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huo. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania umesema utaendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan katika kukomesha  ukatili wa kijinsia hapa nchini. 

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum na waandishi wa Habari kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Balozi  wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kuwa Tanzania imekuwa ikifanya vizuri kwenye masuala ya kijinsia na kwamba Serikali imekuwa ikisimamia vizuri suala hilo.

“Tatizo unyanyasaji wa kijinsia ni jambo la Kidunia na ufaransa imekuwa ikifanya jitihada kubwa kupinga kwa vitendo ukatili wa kijinsia kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi ili waweze kujitegemea kiuchumi na kuondoa mfumo dume ili kuwepo na usawa” amesema.

Amesisiza kuwa ili kuhakikisha ukatili unakomeshwa katika jamii ni lazima kuhakikisha kila mwanamke anajengewa uwezo wa kutambua haki zake sambamba na kumuimasisha kwenye nyanja zote hususani kumiliki uchumi wake.

Wakati huo huo Balozi wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fanti pamoja na Mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja huo, kwa pamoja wamefanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Alliance Française kuwasilisha mpango wa mwaka huu wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia (GBV) nchini Tanzania.

Akizungumza katika mkutano huo Balozi Fanti amesema kuwa Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayolenga kuhamasisha kuhusu athari za ukatili, hasa kwa wanawake na wasichana wadogo nakwamba Kampeni hiyo itaanza rasmi tarehe 25 Novemba, Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, na kuhitimishwa tarehe 10 Disemba, Siku ya Haki za Binadamu. 

“kampeni hii inasisitiza kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake, kwa namna yoyote, ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Kwamba wanawake, wasichana, wanaume na wavulana katika utofauti wao wote wanapaswa kuchukua msimamo dhidi yake” Amesema.

Na kuongeza kuwa “Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya zimeungana na UNFPA na washirika kukomesha unyanyasaji wa kijinsia” Ameongeza.

Amesisiza kuwa Kampeni hiyo ya kimataifa inalenga kuongeza uelewa juu ya  athari za ukatili, hasa kwa wanawake na wasichana wadogo.

“kampeni hii inasisitiza kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake, kwa namna yoyote, ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba wanawake wote, wasichana, wanaume na wavulana katika utofauti wao wote wanapaswa kuchukua msimamo dhidi yake.

Amezitaja Balozi zinazoshiriki kwenye kampeni hiyo ni Ubelgiji, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani,, Ireland, Uholanzi na Uhispania.

Aidha ujumbe wa Umoja wa Ulaya, pamoja na wadau wa kitaifa na UNFPA wataratibu  matukio kadhaa ya umma Jijini Dar es Salaam na Mikoa mingine kuanzia  Novemba 25 hadi Disemba 10, 2021, ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Komesha ukatili wa kijinsia sasa”

Siku ya Disemba 8,2021, ndio itakuwa siku rasmi ya kuhitimisha kazi hiyo ambapo tukio hilo litafanyika kwenye hoteli ya Serena iliyopo Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1 jioni na kusindikizwa na burudani za wasanii mbalimbali mashuhuri Akiwamo  Ben Pol, Nandy, Siti na Bendi, Muziki wa Bedja na Shikandol .

Mwisho.

ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI ZA  MKUTANO HUO. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here