Home BUSINESS ARUSHA DC YATOA MKOPO WA MILIONI 384 KWA WANAWAKE, BIJANA NA WENYE...

ARUSHA DC YATOA MKOPO WA MILIONI 384 KWA WANAWAKE, BIJANA NA WENYE ULEMAVU

 
Mkuu wa wilaya ya ArumeruMhandishi Richard Ruyango akiongea na vikundi vya wanawake vijana na wenye ulemavu walionufaika na mkopo wa milioni 384.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Suleman Msumi akielezea jinsi halmashauri hiyo utakavyo endelea kutekeleza kusudi la serika la kuwewezesha kiuchumi makundi ya wanawake vijana na wenye ulemavu.

NA: NAMNYAK KIVUYO ARUSHA

Halmashauri ya Arusha imetoa fedha, kiasi cha shilingi miloni 384 kwa vikundi 50 vya Wanawake, na Vijana, pamoja na watu wawili wenye Ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kwa halmashauri kutoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa makundi hayo matatu, mikopo isiyo na riba, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya halmashauri hiyo, Mkuu  wa Wilaya ya Aruemru, Mhandisi Richard Ruyango, ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Arusha, kwa kutekeleza kwa vitendo, azimio hilo la Serikali na kuwataka wanavikundi hao kuhakikisha wanatumia fedha hizo kwa malengo waliyokusudia na si vinginevyo.

Amesema kuwa, mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani inatokana na kodi zenu zinazokusanywa na halmashauri yenu kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato, hivyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mjeshimiwa Rais, mama Samia Suluhu Hassan, ikaona ni vema kurudisha asilimia 10 ya mapato yake kwa wananchi kwa kuwapa mikopo isiyokuwa na riba, ili wananchi waweze kunufaika kwa kujipatia mitaji itakayozalisha faida kwa kuongeza kipato cha familia na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo ameshangazwa na idadi ndogo ya vikundi vya vijana ukilinganisha na vikundi 40 vya wanawake vilivyojitokeza kuomba mikopo hiyo, kwa vijana kushindwa kujitokeza kutumia fursa hiyo adhimu inayotolewa na serikali yao, jambo ambalo linaendelea kuzorotesha maendeleo ya vijana nchini, vijana mbao taifa linawategemea.

“Ninawashangaa sana vijana, katika shilingi milioni 384, vikundi vya vijana wanapata milioni 85 tuu, niwasihi vijana wangu, tambueni serikali yenu inawajali, tumieni fursa hii kwa kuchukua hatua ya kujiunga kwenye vikundi ili kupata mikopo hii, anzisheni biashara ndogo ndogo kupitia raslimali zinazopatikana katika maeneo yenu, msiogope kuthubutu vijana wangu” amesistiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Jamii, kuendelea kutoa elimu kwa vijana kwa kuwafikia vijana wengi zaidi katika maeneo yao, ili wapate uelewa juu ya mikopo hii na kujiunga kwenye vikundi vitakavyowawezesha kutumia fursa hii ya kupata mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali yao.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung’u Salekwa, amewasihi wanavikundi hao hasa kina mama, kuwa makini na miezi hii ya sherehe kwa kuacha kushawishika kutumia fedha hizo kwenye sherehe zinazofanyika kila mwisho wa mwaka.

“Mmepokea fedha hizi, kipindi ambacho kuna sherehe nyingi za kufunga mwaka, msije mkatumia fedha hizo kwenye ubarikio, ‘mbesii’ za kina mama, wala kununua vitenge vya ‘wax’ doti 60 kwa ajili ya ‘send off’, tumieni fedha hizo kuzalisha na kujionhezea kipato cha familia pamoja na kurejesha kwa wakati” amesisitiza Mwenyekiti huyu wa Halmashauri.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya  Arusha, Seleman Msumi, licha ya kuwasisitiza wanavikundi hao, kuwa fedha hizo ni za mkopo na si zawadi, amefafanua kuwa katika mapato ya halmashauri kwa kipindi cha miezi mitatu ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022, halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 384 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha zilizokusanywa, kwa ajili ya kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Amebainisha kuwa kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa vikundi 40 vya wanawake waliokopeshwa shilingi milioni 295, vikundi 10 vya vijana waliokopeshwa shilingi milioni 86, na watu wawili wenye ulemavu waliokopeshwa shilingi milioni 4 na kufanya jumla ya shilingi milioni 384.

Hata hivyo wanavikundi hao wameishukuru serikali ya awamu ya sita, kwa kuwajali wananchi wa hali ya chini kwa kuwapa mikopo isiyokuwa na riba huku wakiahidi kwenda kutumia fedha hizo kufanya biashara walizokusudia kwa kuzalisha faida pamoja na kurejesha kwa wakati.

Elibariki Munga aliyepokea mkopo huo kupitia kundi la watu mwenye ulemavu, amethibitisha kuwa mwaminifu katika kurejesha fedha hizo huku akisistiza kurejesha kwa uaminifu fedha alizopokea, kutokana na ukweli kwamba serikali kwa sasa imewathamini sana watu wenye ulemavu tofauti na hapo awali.

“Tutakuwa waminifu katiaka kurejesha mikopo hii, ninaamini kati ya watu ambao watakuwa waaminifu kurejesha fedha hizo ni sisi watu wenye ulema, niaahidi kurejsha fedha hizi kwa wakati bila usumbufu wowote” amethibitisha Munga.





Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TANO NOVEMBA 3-2021
Next articleSTAMICO YAPONGEZWA KUWAKUMBUKA WACHIMBAJI WADOGO WENYE USIKIVU HAFIFU MBEYA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here