Home LOCAL WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MAZISHI YA OLE NASHA

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MAZISHI YA OLE NASHA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William Tate Ole Nasha katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijjii cha Osinoni wilayani Ngorongoro.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwenye mazishi ya aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William Tate Ole Nasha yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijjii cha Osinoni wilayani Ngorongoro.


Baadhi ya viongozi na wananchi walioshiriki kwenye mazishi ya aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William Tate Ole Nasha yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijjii cha Osinoni wilayani Ngorongoro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William Tate Ole Nasha katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijjii cha Osinoni wilayani Ngorongoro


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge Job Ndugai kwenye mazishi ya aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William Tate Ole Nasha yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijjii cha Osinoni wilayani Ngorongoro , Oktoba 2, 20231. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge Ngorongoro na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, William Tate Ole Nasha na amewasihi wananchi wamuenzi kwa kuyaendeleza mambo mazuri yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye ameshiriki katika mazishi hayo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kifo cha Ole Nasha ni pigo kubwa kwa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bunge pamoja na kwa wanafamilia na wananchi wa Ngorongoro.

Mazishi hayo ya Ole Nasha yamefanyika leo (Jumamosi, Oktoba 2, 2021) nyumbani kwake katika kijiji cha Osinoni kata ya Kakesyo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha. Mbunge huyo alifariki Jumatatu, Septemba 27, 2021 mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia anawataka Watanzania waenzi mambo mazuri yote aliyoyafanya marehemu Ole Nasha ili jamii aliyokuwa anaiongoza inufaike. “Marehemu amefanya mambo mengi na ametoa mchango wa hali ya juu kwa Serikali.”

Amesema jambo la muhimu kwa sasa ni kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. “Mke wa marehemu, watoto, ndugu, jamaa na wabunge nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.”

Kwa upande wake, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –Uwekezaji, Geofrey Mwambe amesema Serikali hususani Ofisi ya Waziri Mkuu imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mpiganaji kwa sababu marehemu Ole Nasha alikuwa mtumishi hodari.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Martin Ngoga, viongozi wa Serikali, wabunge pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here