Na: Stella Kessy DAR.
KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Oktoba 4 kimeanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022.
Kikijiandaa na mchezo utakaochezwa Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa katika kuwania kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia wakiwa wapo kundi J.
Hata hivyo mpaka sasa kiungo wa simba Jonas Mkude bado hajaripoti katika mazoezi ya kutokana na matatizo ya kifamilia kwa mujibu wa Meneja wa Stars, Nadir Haroub.Hata hivyo Kocha mkuu Kim Poulsen amewapatia wachezaji program maalumu wachezaji wote ili kuwaweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.
Pia Kibu Denis na Kibwana Shomari ni miongoni mwa wachezaji ambao wameripoti kambini leo na kuanza mazoezi Uwanja wa Mkapa.