Home Uncategorized SIMBA YAREJEA MAZOENI KUELEKEA MCHEZO WAO NA GALAXY

SIMBA YAREJEA MAZOENI KUELEKEA MCHEZO WAO NA GALAXY

Na: Stella Kessy, DAR.

BAADA  ya mapumziko wa siku mbili kikosi kimerejea mazoezini leo kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Jwnaneng Galaxy ya Botswana.

Katika mchezo huo utakaopigwa  Octoba 14-15 nchini Botswana na utakuwa wa kwanza kwa baada ya kumaliza mechi ya timu ya taifa.

Pia wachezaji ambao wataanza mazoezi ni wale ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa huku wale walioitwa ambao wameshaenda kuungana katika timu zao za taifa.

Hata hivyo jumla ya nyota 16 katika kikosi cha simba wameitwa katika timu zao za taifa ambapo wachezaji 9 wapo katika timu ya Taifa Stars na saba ni wale wa timu za kimataifa.

Baada ya kumaliza mechi zao za timu za taifa wachezaji wa kikosi hicho wanahitajika haraka ili kujiunga na wenzao katika mazoezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here