Home SPORTS NYOTA SABA WA SIMBA WAONDOKA NCHINI KUJIUNGA NA TIMU ZAO ZA TAIFA

NYOTA SABA WA SIMBA WAONDOKA NCHINI KUJIUNGA NA TIMU ZAO ZA TAIFA

 Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KIKOSI  cha simba kimesema kuwa nyota wake saba ambao wameitwa katika timu zao za taifa wameondoka leo kwenda kujiandaa na mechi za kufuzu fainal za kombe la Dunia.

Mechi za kwanza zitapigwa Oktoba 7 wakati za marudiano zitakuwa oktoba 10 baada ya hapo.

Huku mshambuliaji meddie Kagere ameitwa katika timu yake ya Taifa Rwanda itakayokutana na Uganda ambapo Taddeo Lwanga naye yupo katika kikosi.




Peter banda na Duncan Nyoni wameitwa kwenye timu yao ya taifa Malawi’ The flames’ ambayo inajiandaa na mchezo dhidi ya ivory Coast.

Joash Onyango atakuwa na timu yake ya taifa ya Kenya ambayo itacheza na Mali.

Kiungo Fundi Rally Bwalya amejumuishwa kwenye kikosi cha zambia kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Afrika ya Kati.

Mlinzi Henock Inonga, Baka pia ameitwa kwenye
Timu ya taifa ya Jamhuli ya Kidemokrasia ya Congo  ambayo itacheza na  Madagasca.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here