NA: HERI SHAABAN.
HALMASHAURI YA JIJI la Dar es Salaam imezindua mafunzo kwa ajili ya kuwapatia Elimu Walimu wake wa Shule za Msingi wa Halmashauri hiyo pamoja kusikiliza changamoto zao.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Afisa Utumishi Mkuu wa Halmashauri hiyo Benedecta Mwaikambo .
Akizindua mafunzo hayo Benedecta alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu wao kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
“Halmashauri yetu leo imeanza kutoa mafunzo kwa walimu wake wa Clasta ya Upanga zaidi ya walimu 500 tunawapa Elimu pia tunasikiliza changamoto za Walimu” alisema Benedecta .
Alisema kazi ya Walimu ni wito hivyo wana jukumu kubwa katika utoaji wa Elimu kwa ajili kuwandaa Taifa bora lenye Elimu katika nchi yetu ya Tanzania na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Aliwataka walimu wa Halmashauri ya Dar es Salaam kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kusimamia sekta ya Elimu ikiwemo kuongeza ufaulu na kukuza taaluma kwa Wanafunzi.
Kwa Upande Kaimu Kaimu Katibu Mkuu Msaidizi Tume ya Watumishi ya Walimu Halmashauri ya Dar es Salaam Subira Mwakibete alisema Walimu wamepandishwa vyeo hivi karibuni baadhi yao mishahara yao bado ile ile ya awali hivyo wana haki ya kuwasikiliza na kupokea changamoto zao.
Subira alisema mafunzo hayo ni endelevu kwa walimu wote watawafikia .
Mratibu wa Magonjwa ya Mlipuko Halmashauri ya Jiji hilo Michael Kweba alitoa Elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona pamoja na kuwapatia chanjo Wali mu waliokuwa tayari kuchanjwa .
Mwisho