Home BUSINESS WAZIRI MKUU ATAKA WATEJA WASIKILIZWE

WAZIRI MKUU ATAKA WATEJA WASIKILIZWE


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa kwanza kushoto) akiwasalimia wadau waliopo katika mabanda mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Maonesho kabla ya kuhutubia.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akihutubia wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi


Meneja Mauzo na Masoko NHC Itandula Gambalagi akifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayumo pichani).
 
Na: Domina Rwemnyila, GEITA.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amezitaka taasisi nchini kuwajali na kuwasikiliza wateja wao. 

Ameyasema hayo leo (22/09/2021) alipokuwa akizundua  Maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji Sekta ya Madini yanayozishirikisha sekta za madini, taasisi za Serikali na Makampuni mbalimbali  katika viwanja vya Bombambili – EPZ Mkoani Geita.   

Waziri Mkuu amesema kuwa baadhi ya taasisi zinaposhiriki kwenye Maonesho wanakuwa na utaratibu mzuri sana wa kupokea na kusikiliza maoni ya wananchi na wengine hutoa namba za simu au barua pepe kwa lengo la kuendelea kuwasiliana na mteja pindi atakapohitaji huduma yao. 

“Inasikitisha sana baada ya kumalizika kwa Maonesho watoa huduma hao hawatoi ushirikiano mzuri kwa mteja kama mbavyo walitoa wakati wa maonesho, kitendo hiki siyo kizuri kwani  ni wewe mwenyewe ulitoa namba zako za simu na kumuhaidi mteja wako ikiwa atahitaji maelezo zaidi awasiliane na ww sasa kwanini hupokei simu wala kujibu barua pepe” Alihoji Waziri Mkuu.

Amezitaka taasisi zote zilizoshiriki Maonesho hayo kuacha tabia hiyo na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo ni kumdanganya mteja na kuonesha ni jinsi usivyojiamini na kazi yako, lakini pia huduma unayotoa ina kasoro. 

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amewapongeza washiriki wote waliojitokeza katika Maonesho hayo kwa kukubali kushiriki na kuonesha shughuli wanazofanya na elimu waliyotoa kwa wanachi ambayo itawasaidia wananchi hao kupata ujuzi na hatimaye kujikwamua kimaisha. 

Kwa upande wake Waziri wa Madini Dakta Dotto Biteko, amezishukuru taasisi za Serikali ambazo zimeshiriki katika Maonesho hayo kwani zimeweza kubadili taswira na muonekano wa Maonesho kwa kuwa wananchi wengi walifikiri wataona madini tu, lakini wameweza kupata huduma nyinginezo kama za sekta ya nyumba. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule, amewashukuru washiriki wote kwa elimu  na ujuzi waliotoa kwa wananchi waliotembelea mabanda hayo kwani wameweza kupitia elimu iliyotolewa na ana Imani itawawezesha kujikwamua kiuchumi na hivyo kuweza kujiongezea kipato. 

Shirika la Nyumba la Taifa – NHC linashiriki Maonesho ya 4 ya Teknolojia na Uwekezaji Sekta ya Madini kwa mwaka huu yameongozwa na kauli mbiu isemayo “Sekta ya Madini kwa Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu”


 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here