Home BUSINESS STAMICO YATOA ELIMU KWA WADAU WA SEKTA YA MADINI NA WACHIMBAJI WADOGO...

STAMICO YATOA ELIMU KWA WADAU WA SEKTA YA MADINI NA WACHIMBAJI WADOGO GEITA

Na: Mwandishi wetu, GEITA.

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesema kuwa kupitia kwenye kituo chake cha Mfano cha wachimbaji wadogo kilichopo eneo la Lwamgasa Mkoani Geita wameweza kuwafikia wachimbaji wadogo zaidi ya 200 kwaajili ya kuwaelimisha na kuwahudumia katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya uchenjuaji.

Hayo yamesemwa na Meneja mwendeshaji wa kituo hicho Victor Augustine kwenye ziara ya wadau wa Sekta ya Madini walipotembelea kituo hicho kwaaajili ya kujifunza na kufahamu namna ambavyo kituo hicho kinavyofanya shughuli zake.

Amesema kuwa Kituo hicho mpaka sasa kimeweza kuwasaidia wachimbaji zaidi ya 200 ambao wamefika kwaajili ya kupata elimu ya kitaalamu kuhusu mambo mbalimbali ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu pamoja na kuwahudumia kwa kuchenjua dhahabu yao kwa gharama nafuu.



“Pamoja na kutoa elimu pia tunachenjua dhahabu zao na kusimamia zoezi zima mpaka hatua ya mwisho ya kukabidhiwa dhahabu yake pamoja na kuwapa ushauri wa kitaalamu kwenye sekta hii ambayo imewasaidia sana na kuendelea kukiamini Kituo chetu” Amesema Victor.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya HEXAD, Fortunatus Luemeja kizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo Mkoani humo ameishukuru STAMICO kuweza kuwajengea Kituo hicho ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwao wa kufanya shughuli zao wakiwa na  uhakika wa kupata dhahabu yenye viwango vya juu na kuweza kuipeleka kwenye soko la dhahabu kulingana na bei elekezi ya soko hilo.



“Kituo hiki ni muhimu sana kwetu sisi wachimbaji wadogo kinatusaidia sana kutokakana na ufanisi wake wa kazi na uwazi kwenye zoezi zima la kuchenjua lakini ipo changamoto ya udogo wa kituo hii inasabibisha kuchukua muda mrefu hadi mwezi mmoja pale unapokuwa na mzigo mkubwa” Amesema Luemeja.

STAMICO ni Shirika la Madini la Taifa lenye majukumu ya kusimamia shughuli za uchimbaji wadogo katika migodi ya Serikali,  kuwalea na kuwaendeleza wachimbaji wachimbaji wadogo pamoja na kufanya utafiti na shughuli za uchorongaji.

MWISHO.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here