Home BUSINESS SERIKALI KUZIIMARISHA TAASISI ZAKE ZA STAMICO NA GST ILI KUENDELEA KUTOA HUDUMA...

SERIKALI KUZIIMARISHA TAASISI ZAKE ZA STAMICO NA GST ILI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA : WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimu wadau mbalimbali alipokuwa akipita kwenye mabanda yao kuona shughuli zao wanazozifanya.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Geita wakati akifungua maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyia kwenye uwanja wa EPZ Mjini Geita.

Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse akifualitilia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwenye sherehe za ufunguzi wa maonesho ya madini Geita.

Kaimu Meneja mgodi  wa STAMIGOLD  Ali Saidi Ali akiwa na Maofisa wa Shirika la Madini laTaifa (STAMICO) wakifualitia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. KassimMajaliwa.

Na: Mwandishi wetu, GEITA.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuimarisha Taasisi zake hususan Taasisi ya Jiolojia Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili taasisi hizo ziweze kutoa huduma bora na nafuu kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na uchorongaji wa miamba ili kujua uwepo na wingi wa mashapo.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akifungua Maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayozishirikisha sekta za madini yanayofanyika Mkoani Geita nakwamba hatua hiyo, itasaidia wachimbaji wadogo kuendesha shughuli zao kwa tija na uhakika na hivyo, kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

“Natoa wito kwa wachimbaji kutumia taasisi hizi ili muweze kupata taarifa za mashapo ya madini na kuchimba kwa uhakika. Katika hili, ninaielekeza Wizara ya Madini kuhakikisha suala la Local Content linasimamiwa kikamilifu. Aidha, makampuni yote makubwa yatumie huduma za GST na STAMICO ispokuwa pale ambapo itathibitika wameshindwa ndipo waagize nje” Amesem mhe. Waziri Mkuu.

Aidha amesema kuwa sekta ya madini imeendelea kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini nakwamba Matarajio ya Serikali ni kuongeza zaidi mchango huo kupitia shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji madini, usanifu madini na utoaji wa huduma katika shuguli za madini.

“Lengo la Serikali ni kufungamanisha ustawi wa sekta ya madini ili uchangie kukua kwa Sekta nyingine za kiuchumi na huduma zikiwemo viwanda, ujenzi, usafirishaji, mawasiliano na nishati” Ameongeza.

Awali Waziri Mkuu alipata nafasi ya kuyatembelea baadhi ya mabanda ya wadau wa sekta ya madini ambapo alipata fursa ya kushuhudia namna wachimbaji wadogo wanavyofanya shuguli zao na hivyo kutoa wito kwa wachimbaji hao na wadau wote kwa ujumla

kutumia vizuri fursa ya maonesho hayo kujifunza na kukutana na wadau mbalimbali wenye uzoefu kwa lengo la kupata suluhisho la changamto zinazowakabili.

Maonesho hayo ambayo yamefunguliwa rasmi leo na Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yanatarajiwa kufungwa siku sya j.pili Septemba 28 mwaka huu. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here