
Na: Mwandishi wetu, MARA.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi mapema leo asubuhi amewaongoza wananchi wa Mkoa huo na watumishi wa kada tofauti wa halmashauri ya Musoma kwenye zoezi la kufanya usafi katika Stendi ya zamani ya mabasi mjini Musoma, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya Usafi Mkoa wa Mara.
Katika zoezi hilo Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Mhe. William Patrick Gumbo na Makamu wake, huku wananchi wa mji huo wakionekana kuwa na mwitikio mkubwa kwenye zoezi hilo.