Home LOCAL NHIF YAKABIDHI KADI KADI ZA MATIBABU KWA WANACHMA 54 MAONESHO YA MADINI...

NHIF YAKABIDHI KADI KADI ZA MATIBABU KWA WANACHMA 54 MAONESHO YA MADINI GEITA

 

Na: Mwandishi wetu, GEITA.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Wilson Shimo leo Septemba 26, 2021 amekabidhi Kadi za Bima ya Afya kwa wanachama 54 waliojiandisha kwenye Banda la Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) wakati wa maonesho ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA-Bombambili mjini Geita.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi kadi hizo Mhe. Mkuu wa Wilaya amewapongeza NHIF kwa kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo wenye manufaa makubwa kwa Afya za watanzania.


“Hongereni kwa kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfuko huu, kwakweli mnafanya kazi nzuri ambayo inaonekana, hii ni sehemu ambayo inatoa ukombozi mkubwa, kwani maradhi huwa hayapigi hodi hivyo unapovamiwa na ugonjwa inasaidia kupata huduma za matibabu.” Amesema.

Aidha, Mhe. Shimo amewataka wachimbaji wadogo, Wajasiriamali na wakulima na wafugaji kupitia vyama vya Ushirika na Bodaboda kujitokeza kwenye Banda hilo na kwenye ofisi za NHIF ili kupata bima kwa zitazowasaidia kutibiwa wanapopata maradhi.

“Bima kwa watoto wadogo ni jambo jema sana kwani watoto hawa kuanzia Sasa wamepata kinga dhidi ya Maradhi na tumeona wachimbaji wadogo wa Madini na vikundi mbalimbali kwenye Halmashauri zetu Wana fursa za kujiunga lakini pia wakulima mbalimbali kupitia vyama vya ushirika na mtu mmoja mmoja ni wakati wao kuja kutumia hii fursa na kupata bima.” Amesisitiza Mhe. Shimo.

Meneja wa Mkoa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ndugu Elias Odhiambo amesema mfuko huo una mpango wa bima ya Afya kwa wajasiriamali wadogo, boda boda na kwamba wana mpango wa bima ya Afya kwa mtu mmoja mmoja na wanafunzi ambapo wamedhamiria kuwafikia kila Mtanzania hivyo hakuna sababu ya mtu yeyote kukosa bima ya afya.

“Banda letu kwa siku 9 za mwanzo limetembelewa na watu zaidi ya 482, wamepata huduma za kupima Afya na wamepata Elimu ya papo kwa papo na walio wengi baada ya kupata Elimu hapa wameenda kujiandaa na wengi waneahidi kuja ofisini kujiandikisha.”

Ndugu Odhiambo amefafanua kuwa ,mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unahudumia wananchi wote na kwamba kuna Makundi mbalimbali ya kutoa huduma hizo.  “Leo tumetoa kadi kwa Makundi mawili ya mpango wa bima ya Afya kwa watoto na kundi mpango wa mtu mmoja, kwenye kipindi hichi Cha maonesho wananchi wengi wametembelea kwenye Banda letu wamepata Elimu wameamua kujiandikisha,” amesema.

“Huduma hii inatusaidia sana inapotokea dharula na hauna fedha inatufanya tupate matibabu hivyo basi leo tunashukuru kupata kadi za matibabu ambapo hatujamaliza hata wiki moja tangia tujiunge na tumepata kadi zetu, natoa wito kwa wengine waje banda la nhif.” Amesema Paulina Lugata, mzazi wa Mtoto Gabrielle.

Previous articleBRELA YAWAHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA 200 NA KUTOA VYETI PAPO KWA HAPO MAONESHO YA MADINI GEITA
Next articleMAYELE APELEKA USHINDI JANGWANI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here