Home BUSINESS TWCC YASHIRIKI MIKUTANO YA ANA KWA ANA KUELEZEA MIKAKATI YAO YA KUWAINUA...

TWCC YASHIRIKI MIKUTANO YA ANA KWA ANA KUELEZEA MIKAKATI YAO YA KUWAINUA WANAWAKE KIBIASHARA

Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wafanyabiashara nchini TWCC Mercy Silla (katikati) akizungumza katika mkutano huo alipokuwa akitoa mada ya namna ambavyo Taasisi yake inavyoshirikisha wanawake kwnye masuala ya kibiashara na ushiriki wao kwenye maonesho hayo. ((PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Badhi ya wadau waliohudhuria kwenye mkutano huo ambao pia ulifanyika kwa njia ya mtandao kuwapa fursa wadau wengine kuweza kuhudhuria kutoka kwenye maeneo yao. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).


Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAM.

Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Mercy Silla amesema kuwa ni muhimu kwa wafanyabishara kuhudhulia mikutano ya ana kwa ana ambayo inaandaliwa na mamlaka ya biashara iliyo chini ya wizara ya viwanda Tantrade ili kupata uewelea zaidi kuhusu Masoko na mahusiano ya kibiashara,


Ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na waandishi wa habari wakati wa mikutano ya ana kwa ana ilyioandaliwa na Tantrade kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam uliokuwa umekutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya nafaka hapa nchi na nje ya Nchi.


Katika mkutano huo ambao pia ulifanyika kwa njià ya Mtandao ili kutoa fursa kwa wadau wengine walio mikoani na nje ya nchi kushiriki Mwenyekiti huyo aliiwakilisha Taasisi yake na kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa nafaka nchini kupata soko la uhakika wa Bidhaa zao.


“Zipo changamoto zinazowakabili wadau wa nafaka na kubwa zaidi ni namna wanavyoweza kupata soko la bidhaa zao ndio maana hapa nimeweza kuwasilisha mada na mchango wetu kama TWCC ili kwa pamoja tuweze kuona namna gani wadau wa nafaka wanaweza kulifikia soko kwani soko lipo ndani na hata nje pia” Amesema Silla.


Aidha ameipongeza Mamlaka ya Tantrade kwa kuendesha mikutano hiyo kwa ufanisi mkubwa huku akiyazungumzia maonesho ya mwakaa kufana na hivyo kuwaomba wananchi wote kufika kwenye Banda la TWCC kujionea Bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali ya juu zinazozalishwa na wakina Mama wa TWCC kote nchini. 


“kimsingi maonesho hadi kufikia leo yanakwenda vizuri na kama mnavyoona hapa kumechangamka na kikubwa wanawake wamejitokeza sana katika maionesho haya jambo ambalo linaleta faraja hususani kwenye Sekta ya Biashara hapa nchini” amesema Mercy.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here