Home LOCAL ZUWENA OMARY JIRI NA DC MSTAAFU CHAULA WAAGWA RASMI SIMANJIRO

ZUWENA OMARY JIRI NA DC MSTAAFU CHAULA WAAGWA RASMI SIMANJIRO

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, akimkabidhi tuzo Katibu Tawala wa Mkoa RAS Shinyanga, Zuwena Omary Jiry kama ishara ya zawadi ya utumishi uliotukuka kwenye nafasi ya Katibu Tawala wa Wilaya DAS Simanjiro iliyotolewa na Chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara, (MAREMA) Tawi .
 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, (kushoto) akimkabidhi tuzo ya utumishi uliotukuka Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro, Mussa Waziri, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya mstaafu wa Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula, iliyotolewa na Chama Cha Wachimbaji madini Mkoa wa Manyara, MAREMA Tawi la Mirerani.

Anaripoti: Gift Thadey, Simanjiro

Wilaya mstaafu wa Simanjiro, mhandisi Zephania Adrian Chaula na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, RAS Zuwena Omary Jiri wameagwa rasmi na chama cha wachimbaji wa madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Tawi la Mirerani na kukabidhiwa tuzo na Mkuu wa Mkoa huo, Charles Makongoro Nyerere.
 

DC mstaafu mhandisi Chaula na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga (RAS Shinyanga Zuwena ambaye awali alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya DAS wa Simanjiro, waliagwa rasmi na MAREMA Tawi la Mirerani kwa kukabidhiwa tuzo na RC Makongoro kwenye tukio la kuwapa tuzo 19 za aina tatu, wamiliki tisa wa migodi ya madini ya Tanzanite katika Mji mdogo wa Mirerani.   
 

Hata hivyo, katika tukio hilo RAS Shinyanga Zuwena alikabidhiwa tuzo hiyo ila DC mstaafu Simanjiro Chaula hakuwepo na tuzo yake ikakabidhiwa kwa Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mussa Waziri.
 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo RAS Zuwena amewashukuru wadau wote, wachimbaji madini, viongozi na wananchi wa Simanjiro kwa ujumla kwa namna walivyofanikisha utendaji kazi wake kipindi akiwa DAS.  
 

Amesema alipata wepesi wa kutekeleza wajibu wake kutokana na umoja, mshikamano na upendo uliokuwepo kwa wananchi na viongozi wa Simanjiro hivyo anawaaga kwa upendo mkubwa na kuwashukuru.
 

“Nawashukuru wote ila Katibu wa MAREMA Tawi la Mirerani Rachel Njau na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Simanjiro Yefred Myenzi, kwa nafasi ya kipekee nawashukuru sana kwa namna mlivyokuwa mnanisaidia kutekeleza maelekezo ya Mkuu wetu wa wilaya,” amesema Zuwena.
 

Amewaahidi kuendeleza mazuri yote kwenye nafasi mpya aliyoipata ya RAS Shinyanga na akamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyomuamini na kumteua katika kushika nafasi hiyo.
 

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, amempongeza RAS Zuwena kwa kuteuliwa na Rais Mama Samia kushika nafasi hiyo hivyo awakilishe vyema huko Shinyanga kwa heshima ya alipotoka.
 

“Utakapofanya kazi zako vizuri ukiwa Shinyanga sifa zitakuja Simanjiro na Manyara kwa ujumla ila ukiharibu utasababisha sisi sote tuonekane kuwa tumeharibu nakusihi usije kutuangusha huko Shinyanga,”amesema Makongoro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here