Home BUSINESS TAASISI ZASHAURIWA KUTUMIA MAABARA ZILIZOPATA CHETI CHA ITHIBATI YA UMAHIRI

TAASISI ZASHAURIWA KUTUMIA MAABARA ZILIZOPATA CHETI CHA ITHIBATI YA UMAHIRI

Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bi.Stella Mrosso akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBS leo Jijini Dar es Salaam.

NA: EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewaasa Taasisi za serikali au binafsi kutumia huduma za maabara zilizopata cheti cha ithibati ya Umahiri.

Ameyasema hayo leo Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bi.Stella Mrosso akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.

Amesema Tanzania kuna maabara arobaini na mbili (42) ambazo zimepata ithibati ya umahiri kutoka SADCAS, ambazo ni maabara za hospital, za upimaji wa vyakula, upimaji maji, chemikali, mafuta ya magari, vifaa vya ujezi, umeme, uhandisi mitambo na maabara za kupima madini.

Aidha Bi.Stella amesema kuwa kwa kutumia huduma zenye Ithibati tutaweza kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN SDGs 2030).

“Ithibati ya umahiri inaweza kutolewa kwa taasisi zinazotoa huduma ya upimaji,(mfano maabara za hospital, maabara za kwenye taasisi za uthibiti ubora, vyuo vya elimu na tafiti, taasisi za kilimo na mifungo)  ugezi, ukaguzi na uthibitishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali ili kujenga imani kwa watumiaji kuwa bidhaa na huduma inafaa kwa watumizi yaliyokusudiwa”. Amesema Bi.Stella.

Pamoja na hayo amesema taasisi zenye Ithibati ya umahiri ni kielelezo kwamba zimetengeneza na zinatekeleza mifumo ya viwango vya kimataifa (international standards) wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kimsingi ili kufikia lengo lililokusudiwa.

Hata hivyo amesema kuwa Viwango vya kimataifa vinavyohusu maswala ya ithibati ni Pamoja na ISO 17025 Matakwa ya umahiri kwa ajili ya maabara za upimaji na ugezi, ISO 15189 Matakwa ya umahiri kwa ajili ya maabara za hospitali, ISO 17020 Matakwa ya umahiri kwa ajili ya ukaguzi, ISO 17065 Matakwa ya umahiri kwa ajili ya uthibitishaji wa bidhaa, ISO 17021 matakwa kwa taasisi zinazofanya kaguzi ya mifumo ya ubora (certification bodies that conduct managements systems audits).

Amesema faida ya ithibati ni pamoja na kupunguza gharama za kufanya biashara (tested once accepted every where), inasaidia kuondoa vikwazo vya biashara, Kuboresha utendaji kwa kutambua vihatarishi na kuviwekea mkakati wa kuvizuia, Kuwezesha utendaji wenye tija na endelevu na pia Inasaidia technology transfer.

Credit – Fullshangwe Blog

Previous articlePROF. MKUMBO ATAKA MIONGOZO YA KUJIKINGA NA CORONA IZINGATIWE WAKATI WOTE WA MAONESHO YA SABASABA.
Next articleSERIKALI KUTOA UJUMBE MAALUM WA MKAKATI WAKE WA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI JIJINI PARIS UFARANSA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here