Home LOCAL TAASISI YA DON BOSCO YAWAPIGA MSASA WALIMU WAO WA VYUO VYA UFUNDI...

TAASISI YA DON BOSCO YAWAPIGA MSASA WALIMU WAO WA VYUO VYA UFUNDI NA SEKONDARI JIJINI ARUSHA.

Walimu wa Don Bosco Tanzania wakiwa katika hatua mbalimbali za mafunzo katika semina ya kuboresha ufundishaji wao uliofanyika mkoani Arusha.
Walimu wa shule za Don Bosco Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja katika semina yao iliyofanyika mkoani Arusha.

NA:NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Taasisi ya Elimu ya Don Bosco iliyo chini ya kanisa Katoliki Tanzania imetoa mafunzo kwa walimu wa vyuo vya ufundi na Sekondari wa Taasisi hiyo ili kuweza kutoa Elimu bora inayohitajika pamoja na kuweza kutoa vijana watakaoweza kuingia katika soko la ajira ndani na nje ya nchi pamoja na kujiajiri wenyewe.

Akiongea na waandishi wa habari katika mafunzo hayo yaliyofanyika Mkoani Arusha mmoja wa wakufunzi Oswad Manyerere anayeshughulika kuwasaidia vijana  wanaosoma katika shule na vyuo  kuendana na soko la ajira amesema lengo Ni kuwaleta walimu wanaofundisha katika Taasisi zao ili kutadhimini mafunzo wanayotoa ili waweza kuendana na soko la ajira.

“Mitaala haibadiliki Kama teknolojia inavyobadilika na sisi tunaandaa vijana wanaoenda kushiriki katika teknolojia ambayo ni ya kisasa zaidi kwahiyo ili kuendana na mabadiliko hayo sisi Kama Taasisi tunajitadhimini katika ufundishaji wetu na utoaji wa elimu tuweze kuendana na mahitaji yalipo katika ulimwengu,”Alisema Manyerere.

Ameleeza  kuwa baada ya kufanya tathimini waliona  kuna maeneo ambayo wanahitaji kuyaboresha ambapo ili maboresho hayo yaweze kuleta tija wameanza na walimu kwa kuwawezesha  kuwa na sifa zinazostahili za ufundishaji wa maeneo hayo na mwisho kufanikiwa kuzalisha vijana watakaoendana na soko la ajira na mabadiliko ya teknolojia.

“Tunaangalia mwenendo wa solo la Ajira nini kinachohitajika katika maeneo ya kazi, tunaongea na waajiri na wanatumbia mahitaji ni yapi na wakati mwingine yanakuwa juu ya mtaala tunaoifanyia kazi lakini tunaleta kwenye vituo vyetu na kuanza kuyafanyia kazi,” Alifafanua.

Kwa upande wake Nyerembe Yunus kutoka Ofisi ya kutoa huduma kwa vijana katika Shule za Sekondari za  Don Bosco amesema kuwa mafunzo wanayoyatoa katika semina hiyo ni ya kumwezesha mwalimu kutoa elimu iliyo bora na sio bora elimu kwa vijana wao wa Sekondari.

“Shirika letu limejikita katika kutoa elimu iliyo bora ndio maana tuafanya mafunzo haya kwa kuzingatia kwamba mitaala yetu ya masomo inabadilishwa kila baada ya miaka mingi wakati dunia ya Leo kuna mabadiko makubwa sana ya elimu ambayo yanakenda,” Alisema Nyerembe.

Amefafanua kuwa mbali na mitaala iliyopo wanajiongeza ili kuhakikisha kwamba wanaendana na hali halisi ya dunia na wanaamini mafunzo hayo yataenda kuboresha utendaji  kazi wa walimu katika vyuo vyao na shule zao  za sekondari.

“Tuna mikakati ya makusudi ya kuhakikisha kwamba tunayakazia masomo ya sayansi katika shule zetu japo shule zetu zinafanya vizuri lakini hatujaridhika tunaendelea kuboresha zaidi ili kijana anapotoka somo la sayansi linakuwa limemuingia vizuri hasa kwa vitendo,”Alifafanua.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here