Home LOCAL PROF. MKUMBO ATAKA MIONGOZO YA KUJIKINGA NA CORONA IZINGATIWE WAKATI WOTE WA...

PROF. MKUMBO ATAKA MIONGOZO YA KUJIKINGA NA CORONA IZINGATIWE WAKATI WOTE WA MAONESHO YA SABASABA.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo(wa pili kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania  (Tan Trade) Edwin Rutageruka (kushoto) wakati wa ziara fupi aliyoifanya leo kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza leo katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. (katikati) ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dotto James.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa (Tan Trade) Edwin Rutageruka (kushoto) wakiwa katika Banda la Viwanda na Biashara kuangalia katika Maonesho hayo yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (wa pili kushoto) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika moja ya Taasisi zinazoshiriki Maonesho hayo.

Na: Mwandishi wetu, DAR.

RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 45 ya biashara  ya Kimataifa yanayofanyika  katika viwanja vya maonesho Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake fupi kwenye maonesho hayo Waziri wa viwanda na biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo utafanyika Julai 5, mwaka huu. 

“Tunaomba Wananchi wajitokeze Kwa wingi ili kuja kumuunga mkono Rais na wao kuweza kupata fursa ya kutembelea Maonesho haya ya 45  ,na kama nilivyosema  julai 5 kuanzia saa nane mchana mgeni rasmi atakuwa kwenye viwanja hivi..”amesema Prof. Mkumbo. 

Amesema kuwa mandalizi ya maonesho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Uchumi wa Viwanda Kwa Ajira na Biashara endelevu’ yamekamilika na kwamba washiriki 3002 wamethibitisha  kushiriki huku nchi 7 za kigeni zikithibitisha kushiriki yakiwemo makampuni 76.

Akizungumzia ratiba za shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika maonesho hayo Prof. Mkumbo amesema kuwa kutakuwa na uzinduzi wa mfumo wa taarifa za biashara ambao utaongeza uwazi  wa taratibu  za biashara kimataifa ambapo utaongeza wigo wa taarifa  za biashara, pia kutazinduliwa Duka la kimtandao kwa ushirikiano wa Tantrade na Shirika la posta. (Mobile Shop).

Sambamba na hilo Prof. Kitila ameongeza kuwa kutafanyika  uzinduzi wa kutambua  mabanda ya washiriki  wa ndani ya uwanja Kwenye maonesho  hayo ambapo kumeandaliwa ramani ya kuonesha maeneo yaliyopo mabanda ili wananchi waweze kujua mahali anapotaka kwenda kulingana na Banda husika analolihitaji.

Aidha amewataka wananchi kuendelea kuchukua taadhali za kujinga na wimbi la corona kwa kufuata miongozo mbalimbali ya wizara ya Afya  huku akitaja viingilio kuwa ni 1000 kwa watoto na wakubwa 3000 ambapo kwa siku yenyewe ya sabasaba kiingilio kitakuwa 4000 kwa wakubwa na watoto 1000

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here