Home LOCAL MWENYEKITI TAMWA ATAKA WADAU KUSAIDIA UJENZI KITUO CHA JINSIA ZANZIBAR

MWENYEKITI TAMWA ATAKA WADAU KUSAIDIA UJENZI KITUO CHA JINSIA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa TAMWA Joyce Shebe akiwa pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kushoto Shifaa Said Hassan kulila ni mkuu wa kitengo cha uhasibu wa TAMWA upande wa Zanzibar Mohamed Khalid wakipanda ngazi wakati walipokagua ujenzi wa kituo cha jinsia Tunguu Wilaya kati Unguja.

Mwenyekiti wa TAMWA Joyce Shebe akiwa pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kushoto Shifaa Said Hassan kulila ni mkuu wa kitengo cha uhasibu wa TAMWA upande wa Zanzibar Mohamed Khalid wakipanda ngazi wakati walipokagua ujenzi wa kituo cha jinsia Tunguu Wilaya kati Unguja.
Mwenyeki wa TAMWA Joyce Shebe akiwa eneo la ndani linaloendelea na ujenzi katika kituo cha jinsia kinachongwa na Chama hicho huko Tunguu Wilaya ya kati Zanzibar.

ZANZIBAR.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania ( TAMWA ) Joyce Shebe amesema uanzishwaji wa kituo cha jinsia na chama hicho visiwani Zanzibar utaleta tija kubwa kwa manufaa ya jamii nzima na Serikali yake..

Aliyasema hayo wakati alipotembelea ujenzi wa jengo hilo Tunguu Wilaya ya kati Unguja na kueleza kuwa wanachama wana kila sababu ya kujivunia uanzwaji wa kituo hicho.

Alisema kwa miaka mingi tangu kuundwa kwa Chama hicho hakujawahi kufanyika uwekezaji mkubwa wa aina hio na kwamba kufanyika kwake bila shaka kuna nguvu kubwa ambayo inaendelea  kuwekezwa na inahitaji kuendelezwa.

Alieleza kuwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wananchi wanakabiliwa na changamoto kubwa ya elimu ya jinsia kiasi cha kwamba miongoni mwao hujikuta wakingia kwenye matatizo ambayo sababu zake ni ukosefu wa elimu sahihi.

Aliesema kukamilika kwa ujenzi huo ni wazi kuwa kutatua fursa kwa wananchi  wa Zanzibar kujifunza elimu ya jinsia ambayo uewekezaji wa elimu hio anaamini itasambaa na kusaidia wengine hatimae elimu hio kuleta jamii yenye mabadiliko na kutambua umuhimu wa usawa wa kijinsia.

Sambamba na hilo alitoa wito kwa jamii na taasisi mbali mbali za binafsi na Serikali kujitokeza kuunga mko ujenzi huo kwa kutoa misaada kwani ujenzi huo unahitaji zaidi nguvu ya wahisani ili uweze kukamilika.

Awali Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa jingo hilo Shifaa Said Hassan alisema ujenzi huo umeanza mwezi januari mwaka huu na hadi kufikia sasa zimetumika 358,000,000 na asilimia 99 ya gharama hizo zimebebwa na chama hicho wenyewe upande wa Zanzibar.

Hata hivyo alisema ili jengio hilo liweze kukamilikwa alau kwa ghorofa ya kwanza na kuweza kutumika kunahitajika fedha za kitanzania zipatazo 570,297,000 ambazo kwa sasa wasingeweza kumudu gharama hio na kuwataka wahisani waweze kusaidia wakitambua kuwa elimu ya jinsia ni muhimu kwa kila mwananchi kwenye jamii.

Alitoa wito wananchi kujitokeza kusaidia ujenzi huo kwa kiasi chochote kile alicho na uwezo nacho kwani  hakuna kidogo kisichofaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here