DODOMA.
Dkt.Godwin Mollel,Naibu Waziri-Afya leo amezindua rasmi mradi wa uboreshaji wa huduma za Mama na Mtoto na damu salama Mkoani Dodoma, ikiwa lengo kuu ni kuokoa maisha na kupunguza vifo vya akina Mama vitokanavyo na uzazi pamoja na kupunguza vifo vya Watoto. Mradi huu ambao una thamani ya jumla ya USD7,000,000 ambayo ni sawa na Billioni 16.1 fedha za Kitanzania.
Serikali inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika la KOICA, pamoja na Shirika la UNICEF kwa kufadhili mradi huu.