Home LOCAL DKT. GWAJIMA AZUNGUMZA NA SHIRIKA LA PCI.

DKT. GWAJIMA AZUNGUMZA NA SHIRIKA LA PCI.

DODOMA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na kufanya mazungumzo na shirika lisilo la Kiserikali 
la Project Concern International (PCI) linalojishughulisha na huduma mbalimbali za kijamii katika Mkoa wa Mara kwenye Ofisi za wizara jijini Dodoma

Shirika la PCI imekuwa ikijishughulisha na huduma mbalimbali zinazowalenga wanafunzi wa shule za msingi katika Halmashauri 4 za Mkoa wa Mara (Butiama DC, Bunda DC, Bunda TC, na Musoma DC). Jumla ya shule za msingi 231 (ambayo ndiyo idadi ya shule zote za msingi katika Halmashauri zote 4) zimenufaika na huduma zinazotolewa na PCI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here