Home LOCAL DKT, DUGANGE ASHIRIKI UZINDUZI WA NYIMBO ZA DINI KWA LUGHA YA KIBENA...

DKT, DUGANGE ASHIRIKI UZINDUZI WA NYIMBO ZA DINI KWA LUGHA YA KIBENA KKKT ILEMBULA WILAYANI WANGING’OMBE.

 


 Na: Maiko Luoga NJOMBE,
Mbunge wa jimbo la Wanging’ombe, Mkoani Njombe na Naibu Waziri OR-TAMISEMI Dkt, Festo Dugange, Juni 06, 2021 alialikwa kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyimbo za injili zilizoimbwa na Kwaya ya EBENEZA Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania KKKT Usharika wa Ilembula Wilayani Wanging’ombe.
Kwaya hiyo iliyoanza rasmi kutangaza Injili tangu mwaka 1953 hadi sasa, Waimbaji wake ni wenye umri wa kati ya miaka 80 hadi 104 wakiendelea kuimba nyimbo nzuri kwa lugha ya Kibena ambazo zipo kwenye album hiyo.
Hafla hiyo iliambatana na changizo la fedha kwaajili ya kununua mashine ya kukamua mafuta ya alizeti ili kuiwezesha kwaya hiyo kueneza injili, jumla ya fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 6 na laki 2 zilipatikana kati ya hizo Mhe, Dugange alitoa kiasi cha Shilingi Milioni 1 na laki 2 na ahadi za washiriki wengine ilikuwa kiasi cha Shilingi milioni 2.
Ibada hiyo iliongozwa na Mhashamu Baba Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini  Dkt.George Mark Fihavango na Mkuu wa jimbo la KKKT Ilembula Mchungaji Mexon Mng’ong’o.
Aidha katika uzinduzi huo, Mhe, Mbunge Dkt, Dugange aliwapongeza Waimbaji wa Kwaya ya Ebenezer kwa kumsifu na kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji licha ya umri wao mkubwa, huku akiwapongeza Waumini wa Kanisa hilo usharika wa Ilembula na Dayosisi ya kusini kwa ujumla kwa malezi ya kiroho katika jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here