Home LOCAL NITAWATETEA NA KUWAPIGANIA WANANCHI-UMMY MWALIMU

NITAWATETEA NA KUWAPIGANIA WANANCHI-UMMY MWALIMU

Na: Saimon Mghendi,Kahama

Wajasiriamali wa eneo la viwanda la Zongomela lililopo katiaka Manispaa ya Kahama, Mkoani Shinyanga, Wamelalamikia wakala wa misitu wa wilaya ya kahama (TFS) kwa kuwakamata na mbao zao kinyume na utaratibu jambo ambalo hupelekea kupata hasara kubwa.

Wajasiriamali hao wameyasema hayo leo katika ziara ya waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu, alipofika katika eneo la viwanda la Zongomela kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wajasiriamali hao ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani shinyanga.

Akijibu malalamiko hayo Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema kuwa ni jambo ambalo halikubaliki kuona wakala wa Misitu TFS wakiacha kuzuia utoroshaji wa mazao ya misitu maeneo husika badala yake wanakuja kuwasumbua wananchi.

“Hao wanaotorosha Mbao wakamateni huko huko lakini mnasubiri mbao ikishafika dukani ndo mnasema mnatafuta mbao ya wizi, Hapana kwenye hili nitawatetea na kuwapigania na kilio chenu nakipeleka kwa Waziri wa maliasili Dkt. Damasi Ndumbaro”, ailisema Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba, amesema wananchi wanamalalamiko mengi kwa wakala wa misitu wilaya ya kahama TFS, na kuongeza kuwa jambo hilo atalipeleka bungeni ili kuangaliwa upya kwa namna ya kuboresha  sheria hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here