Home SPORTS MKE WA CLATOUS CHAMA AFARIKI DUNIA.

MKE WA CLATOUS CHAMA AFARIKI DUNIA.

LUSAKA, ZAMBIA

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Simba ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa nchini Zambia Clatous Chota Chama amepata pigo baada ya mkewe Mercy Munuka Chama kufariki dunia leo Mei 29,mwaka huu wa 2021.

Mkewe Chama amefariki nchin Zambia na tayari wadau mbalimbali wa soka katika nchi za Tanzania na Zambia zimetoa pole kwa Chama na familia yake kutokana na msiba huo.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Klabu ya soka ya Lusaka Dynamos Rabecca Mumba amesema bodi pamoja na wachezaji wa klabu hiyo kwa  ujumla  wamesikitishwa na taarifa za kifo  huyo hicho.

Chamw aliyewahi kuwa kiungo wa Klabu hiyo tayari yuko nchini humo kutokana na kupatwa na msiba huo mzito.

Mumba amesema Klabu ya Lusaka Dynamos inatoa pole kwa wafiwa sambamba na AIiyekuwa Nahodha wetu. Mioyo yetu ipo pamoja na Familia za wafiwa.”Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu”

Hata hivyo hadi sasa bado haijawekwa wazi chanzo cha kifo chake.

Credit – Fullshangwe Blog

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here