(Picha zote na Ofisi ya Msajili wa Hazina).
Na: Richard Mrusha, ARUSHA.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba ameagiza mashirika ya umma yasiyozingatia mwongozo wa bajeti hususani fedha za maendeleo yachambuliwe na kusitishwa miradi yote itakayoshindwa kukidhi matakwa ya mwongozo wa bajeti kwa mwaka 2012/22
Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,Dk,Khatibu Kazungu kwaniaba ya Waziri wa Fedha,katika ufunguzi wa mafunzo ya mikataba ya utendaji kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Bodi za Taasisi,Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali
Dk,Kazungu amesema zipo baadhi ya taasisi na mashirika ya umma hayazingatii bajeti na kuhakikisha sheria ya bajeti namba 11 ya mwaka 2015 na kanuni zake zinafuatwa hivyo taasisi zisizozingatia mwongozo wa bajeti alimwagiza Msajili wa Hazina,Athumani Mbuttuka kuzichambua upya na kusitishwa miradi yote itakayoshindwa kukidhi matakwa ya mwongozo wa bajeti
Amesema pia maombi ya fedha au idhini ya mikopo kwa taasisi na mashirika ya umma yote yapitishwe kwa msajili wa hazina kwaajili ya kufanyiwa uchambuzi wa maandiko husika kabla ya kuwasilishwa
Amesema taasisi zinapaswa kuwasilisha Ofisi ya Msajili wa Hazina taarifa za utekelezaji za robo mwaka na ndani ya muda uliopangwa ili uchambuzi uweze kufanyika kwa muda na hatimaye ushauri utolewe
“Msajili wa hazina chukua hatua stahiki kwa taasisi zote zinazoshindwa kuwasilisha taarifa kwa mujibu wa sheria zikiwemo zile ambazo serikali wanaziomba kupitiw ofisi “
Pia matumizi ya bodi za wakurugenzi za taasisi yafuate miongozo iliyotolewa na serikali kupitia ofisi ya msajili na kuongeza kuwa taasisi ziwe na Mpango madhubuti wa kuwajengea uwezo watumiaji wa vitengo vya ukaguzi ili wapate uelewa mzuri katika kaguzi
Awali,Naibu Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka amesema mafunzo hayo yameshirikisha washiriki 711 kutoka taasisi,mashirika ya umma na Wakala wa serikali 237 yaliyo chini ya ofisi ya msajili wa hazina na yamejumuisha makatibu wa bodi zwahasibu pamoja na maafisa mipango na yanafanyika Mei 17 Hadi 12 mwaka hapa
Amesema ofisi hiyo imesaini mikataba ya utendaji Kazi kwa taasisi 237 zilizotekeleza matakwa ya kisheria ikiwemo kujenga uelewa kwa washiriki juu ya dhana ya mikataba ya utendaji Kazi pamoja na kuandaa rasimu ya mkata wa utendaji kwa Lila taasisi kwa mwaka 2021/22
Mwisho.