Home SPORTS AZAM FC YAIPIGA BIASHARA UTD 2-0

AZAM FC YAIPIGA BIASHARA UTD 2-0

DAR ES SALAAM.

AZAM FC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na Prince Dube Mpumelelo dakika ya 11 na Mudathir Yahya Abbas dakika ya 54 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 30, ingawa wanabaki nafasi ya tatu, wakizidiwa pointi moja na Yang A SC ambayo pia ina mechi moja mkononi.

Biashara United kutoka Musoma mkoani Mara, yenyewe inabaki na pointi zake 45 za mechi 30 sasa katika nafasi ya nne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here